Trump asema Obama alikuwa akidukua simu yake


Donald Trump amlaumu Obama kwa kudukua simu yake
Image captionDonald Trump amlaumu Obama kwa kudukua simu yake
Rais wa Marekani Donald Trump amemshutumu mtangulizi wake kwa kudukua simu yake mwezi mmoja kabla ya kuchaguliwa kuliongoza taifa hilo.
Rais Trump alichapisha ujumbe wa Twitter mapema siku ya Jumamosi akisema: Makosa sana! Nimegundua kwamba rais Obama alikuwa akidukua simu yangu katika afisi yangu iliopo Trump Tower kabla ya mimi kupata ushindi .
Hawakupata kitu.Hii inaitwa McCarthyism!"{ kutumia njia mbaya kumchunguza mtu}.
Ujumbe wa Twitter uliochapishwa na Trump
Image captionUjumbe wa Twitter uliochapishwa na Trump
Aliongezea kwamba awali mahakama moja ilipinga uchunguzi kuhusu kudukuliwa kwa simu yake.
Rais Donald Trump na Obama
Image captionRais Donald Trump na Obama
Rais huyo wa Marekani hajatoa ushahidi wowote ili kuthibitisha madai hayo ama hata kusema ni agizo gani la mahakama alilonukuu.
Ripoti za vyombo vya habari zimesema kuwa shirika la kijasusi la FBI liliomba agizo la kuwachunguza maafisa wa karibu wa Rais Trump kutoka kwa shirika la kigeni la kijasusi Fisa kubaini iwapo wamekuwa wakiwasiliana na maafisa wa Urusi.
Agizo hilo lilikataliwa lakini baadaye likakubaliwa mwezo Oktoba kulingana na ripoti hizo za vyombo vya habari.
Hakujakuwa na thibtisho rasmi na pia haijulikani iwapo hatua hiyo ilichunguzwa.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment