Shambulio la bomu lauwa maafisa Iraq


Mashambulizi kama haya yamekua yakitokea mara kwa mara Iraq
Image captionMashambulizi kama haya yamekua yakitokea mara kwa mara Iraq
Maafisa wa Iraq wamesema watu wasiopungua 15 wameuawa katika mashambulizi ya bomu kwenye lori kusini mwa mji mkuu, Baghdad.
Zaidi ya watu 45 wanasemekana kujeruhiwa.
Gari hilo lililipuliwa katika kituo cha ukaguzi cha Polisi na miongoni mwa waliouwawa ni baadhi ya maafisa.
Hakuna kundi lililokiri kuhusika na shambulio hilo lakini IS imekua ikifanya mashambulizi kama haya mara kwa mara baada ya kupoteza maeneo waliokua wakishikilia sehemu mbalimbali za Iraq.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment