Mwanasheria mkuu US atakiwa kujiuzulu kwa kuwasiliana na Urusi


Mwansheria mkuu Jeff Sessions kulia ametakiwa kujiuzulu kwa kuwasiliana na Urusi
Image captionMwansheria mkuu Jeff Sessions kulia ametakiwa kujiuzulu kwa kuwasiliana na Urusi
Mwanasheria mkuu nchini Marekani jenerali Jeff Sessions alikutana na balozi wa Urusi wakati wa uchaguzi licha ya kuthibitisha kuwa hakufanya mawasiliano yoyote na Urusi.
Idara ya haki ilithibitisha kuwa alikutana na Sergei Kislyak mnamo mwezi Julai na Septemba mwaka uliopita ikiwa ni miongoni mwa majukumu yake katika kamati ya bunge la seneti ya huduma za usalama.
Bw Session alisema kuwa matamshi yake yalifananishwa na jukumu lake katika kampeni ya rais Trump.
Madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani yamemkabili rais Trump.
Sergei Kislyak wa Urusi
Image captionSergei Kislyak wa Urusi anadaiwa kukutana na Jeff Sessions
Idara ya ujasusi inaamini kwamba udukuzi unaodaiwa kufanywa na Urusi dhidi ya mgombea wa chama cha Democrat Hillary Clinton ulifanywa ukiwa na lengo la kumsaidia bw Trump kumshinda Clinton.
Mshauri wa maswala ya usalama wa rais Trump Michael Flynn alifutwa kazi mwezi uliopita baada ya kuidanganya ikulu kuhusu matamshi yake na bw Kislyak, kuhusu vikwazo dhidi ya Urusi
BBC
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment