Mke wa mgombea uraisi Ufaransa kuchunguzwa


Fillon amesema wapinzani wake wanajaribu kumtumia Penelope kumuangusha katika mbio za urais
Image captionFillon amesema wapinzani wake wanajaribu kumtumia Penelope kumuangusha katika mbio za urais
Mke wa mgombea wa urais wa Ufaransa Francois Fillon amewekwa chini ya uchunguzi kufuatia tuhuma za udanganyifu na ufisadi.
Jambo hili linahusishwa na jukumu la Penelope Fillon kama msaidizi wa mumewe katika shughuli za bunge, ambapo alilipwa maelfu ya dola, lakini inadaiwa kuwa alifanya kazi ndogo na kuwa pesa aliyolipwa haikuwa kwa ruhusa ya bunge.
Fillon anasema kuwa uchunguzi huo umetegeshwa wakati muafaka kwa makusudi ili kuweza kuharibu matumaini yake ya kushinda uraisi.
Raundi ya kwanza ya uchaguzi uko ndani ya muda wa wiki tatu na nusu wiki kutoka sasa.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment