Milio ya risasi yasikika nje ya Bunge Uingereza


Hivi punde
Taarifa zinasema kumetokea milio kadha ya risasi nje ya majengo ya Bunge la Uingereza.
Eneo hilo kwa sasa limefungwa na watu hawaruhusiwi kutoka wala kuingia.
Wanasiasa na wanahabari wamekuwa wakiandika kwenye Twitter kwamba wamesikia milio mikubwa nje ya majengo hayo.
Walioshuhudia wanasema wamewaona watu kadha wakipokea matibabu.
Baadhi ya walioshuhudia wanasema wamemuona mtu akiwa na kisu katika bustani ya majengo ya bunge.
Afisa wa polisi ameambia mhariri wa BBC wa masuala ya siasa Laura Kuenssberg kwamba kuna mtu aliyepigwa risasi nje ya Jumba la Portcullis.
bbc
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment