Afrika yajipatia anwani yake ya mtandao


Bara la Afrika sasa lina anwani yake ya mtandaoHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBara la Afrika sasa lina anwani yake ya mtandao
Bara la Afrika sasa lina anwani yake ya mtandao .africa sawa na ule wa .com kufuatia uzinduzi wake rasmi na muungano wa Afrika AU.
Mwenyekiti wa tume ya umoja huo Nkoszana Dlamini alipongeza uzinduzi wake kama wakati ambapo Afrika imejipatia utambulisho wake wa kidijitali.
AU inasema kuwa anwani ya .africa utalileta pamoja bara la Afrika kama jamii ya mtandao.
Anwani hiyo sasa itaonyesha maslahi ya makampuni barani Afrika.
Kwa mfano kampuni ya simu inaweza kuanzisha anwani yake ya mobile.africa ili kuonyesha uwepo wake barani Afrika.
Icann, kampuni inayotengeza anwani hizo iliiidhinisha hatua hiyo baada ya AU kuwasilisha ombi.
Kampuni hiyo iliongozwa na kampuni ya Afrika Kusini ZA Central Registry ambayo itahusika na usajili wa majina ya .africa.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment