Trump mbioni kumtafuta mshauri wa ulinzi


Donald Trump
Image captionDonald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump anajiandaa kuwafanyia mahojiano wale wanaotarajiwa kuchukua wadhifa wa mshauri wa masuala ya ulinzi wa Marekani, kufuatia kujiuzulu kwa Michael Flynn.
Wale ambao wanatarajiwa kuhojiwa ni pamoja na balozi wa zamani wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa John Bolton na aliye sasa kaimu mshauri Keith Kellogg.
Majemedari wengine wawili ni H.R McMaster na Robert Caslen, pia wamo katika orodha hiyo.
Michael Flynn alijiuzulu Jumatatu ya juma lililopita, kutokana na utata kuhusiana na vikwazo vya Marekani kwa Moscow uliomzingira baada ya kukutana na balozi wa Urusi jijini Washington.
Michael Flynn alijiuzulu Jumatatu
Image captionMichael Flynn alijiuzulu Jumatatu
Donald Trump ametetea mafanikio ya uongozi wake kama Rais wa Marekani, katika mkutano na wafuasi wake huko Florida.
Alisema kuwa alifika Florida, kwa sababu alitaka kuwa karibu na marafiki wake na watu wake wa karibu.
Bwana Trump kwa mara nyingine tena alivishambulia vyombo vya habari, huku akiwalaumu waandishi habari kwa kusambaza taarifa za uwongo, wakiwa na ajenda zao fiche.
BBC
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment