Rais Kenyatta aruka majoka na kudensi na Vijana wa FBI...wengi wamkosoa na kusema ni kampeni

 

Rais Kenyatta akicheza densi iliozua hisia kali miongoni mwa WakenyaHaki miliki ya pichaIKULU
Image captionRais Kenyatta akicheza densi iliozua hisia kali miongoni mwa Wakenya
Video ya Rais Uhuru Kenyatta akicheza densi mtindo wa dab, pale alipokutana na kundi moja la wachezaji densi katika Ikulu ya Nairobi siku ya Jumatano, imesababisha malumbano makali katika mitandao ya kijamii.
Mtandao wa kijamii wa Rais Uhuru Kenyatta ukiwa na picha za densi ya DabHaki miliki ya pichaTWITTER
Image captionMtandao wa kijamii wa Rais Uhuru Kenyatta ukiwa na picha za densi ya Dab
Bw Kenyatta anaendelea na kampeni ya kutaka kuchaguliwa tena Rais kwa muhula wa pili wa miaka mitano, na amekuwa akizuru kote nchini humo, kuwarai vijana kujiandikisha kama wapigaji kura, kabla ya kumalizika kwa kampeini hiyo ya mwezi Februari 15.
Amekuwa akikutana na watu mashuhuri na wasanii wa muziki, kusaidia mikakati yake ya kupata kura dhidi ya wapinzani wake.
Watu wamekuwa wakitumia #DabOfShame, kumkosoa rais huyo, wakisema analenga tu kuimarisha kampeini yake, ilihali taifa hilo liko katika lindi la matatizo chungu nzima, ikiwemo mgomo wa muda mrefu wa madaktari na wahudumu wa matibabu.
Wafuasi wake wanasema kuwa, anaonesha kuwa ni mtu wa kufikiwa kwa urahisi.
Mchoraji vibonzo mmoja nchini Kenyas Victor Ndula, pia ameongeza hili:
Kibonzo cha Victor NdulaHaki miliki ya pichaTWITTER
Image captionKibonzo cha Victor Ndula
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment