Polisi watibua shambulizi la kigaidi Ufaransa


Polisi wa kupambana na ugaidi walivamia nyumba eneo la MontpellierHaki miliki ya pichaAFP
Image captionPolisi wa kupambana na ugaidi walivamia nyumba eneo la Montpellier
Njama ya kufanya shambulizi nchini Ufaransa umetibuliwa huku washukiwa wanne wakikamatwa eneo la Montpellier, kwa mujibu wa waziri wa mambo ya ndani Bruno Le Roux.
Wanaume watatu na msichanawa umri wa miaka 16 walipatikana na bidhaa za kutengeneza bomu na kikosi cha kupambana na ugaidi, wakati wa uvamizi kweye nyumba moja kusini mwa mji.
Vilipuzi vya kutengezewa nyumbani sawa na vile vilivyotumiwa wakati wa shambuliki la mji wa Paris Novemba 15 vilipatikana.
Ripoti zinasema kuwa msichanna alikuwa ameandika ujumbe wa itikadi kali mtandaoni.
Tangu mwanzo wa mwaka 2015, takriban watu 230 wameuawa kwenye mashambulizi nchini Ufaransa.
Ufaransa
Image captionUfaransa
Wiki iliyopita mwanajeshi mmoja alipata majeraha madogo, wakati mwanamme moja aliyekuwa na panga alipojaribu kuingia makavazi ya mjini Paris.
Mwanamume huyo raia wa Misri mwenye umri wa miaka 29 Abdullah Hamamy, alipigwa risasi na kujeruhiwa vibaya
Ripoti za awali zilisema kuwa mmoja wa washukiwa wa Montpellie, huenda akawa mshambuliaji wa kujitoa mhanga.
Shirika moja la habari la Ufaransa lilisema kuwa watu hao wanne, walikuwa wakipinga kushambulia eneo wanakotembea watalii mjini Paris, lakini taarifa za polisi zililiambia shirika la habari la Reuters kuwa uchunguzi haujabaini hasa ni wapi walikuwa wamelenga kushambulia.
Polisi walivamia nyumba moja ambapo walipata vifaa vya kutengeneza mabomuHaki miliki ya pichaAFP
Image captionPolisi walivamia nyumba moja ambapo walipata vifaa vya kutengeneza mabomu
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment