Nyangumi wengine 240 wakwama ufukweni New Zealand


Nyangumi waliofariki katika ufukwe wa bahari nchini New ZaalandHaki miliki ya pichaAFP
Image captionNyangumi waliofariki katika ufukwe wa bahari nchini New Zaaland
Wana mazingira nchini New Zealand, wanasema nyangumi wengine mia mbili na 40 wa aina ya "pilot", wamekwama katika ghuba ilioko mbali, kwenye kisiwa cha kusini cha New Zealand.
Kundi hilo jengine la nyangumi lilikwama kwenye ufukwe unaoitwa Farewell Spit, punde baada kundi la nyangumi mia moja kusaidiwa kurudi baharini maji yalipojaa.
Nyangumi mia tatu walikufa jana.
Eneo hilo la pwani la kilomita 20, lenye maji ya kina kifupi, ni gumu kwa nyangumi kuogelea.
Mamia wajitokeza kuwaokoa nyangumi waliokwama New Zealand
Indaiwa kuwa huenda nyangmi hao walisukumwa hadi ufukweni na papa baada ya alama za kung'atwa kupatikana katika mmojawapo wa nyangumi hao aliokufa.
Hathivyo haijulikani ni kwa nini nyangumi hao wanaendelea kuwasili katika ufuo huo wa kilomita 5 karibu na Golden Bay.
NyangumiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionNyangumi
Wataalam wanasema kuwa nyangumi ambao hujipata ufukweni hutoa wito kwa wenzao ambao nao pia hujipata katika ufukwe.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment