Marekani kuunda ndege mpya za kivita


Ndege ya F-35Haki miliki ya pichaLOCKHEED MARTIN
Image captionNdege ya F-35
Idara ya ulinzi nchini Marekani itanunua ndege zingine aina ya F-35 kutoka kwa kampuni ya kuunda ndege ya Lockheed Martin, kwa bei ya chini kidogo kuliko ya awali.
Mwezi Disemba rais mpya wa Marekani Dolald Trump alisema kuwa gharama ya mpango wa ulinzi wa ilikuwa kumbwa kupindukia.
Kandarasi hiyo mpya ya ndege 90 itagharamu dola milioni 95 kwa kila ndege kutoka dola mlioni 102 .
Ndege ya F-35
Image captionNdege ya F-35
Serikali ya Marekani inatarajia kutumia dola bilioni 400 miongo inayokuja kuunda ndege 2,443 za kivita.
Hisa kwenye kampuni ya Lockleed zilishuka baada ya Trump kulalamikia gharama ya ndege lakini hata hivyo zimepanda tena.
Serikali ya Uingereza nayo ina mpango wa kununua hadi ndege 138 za F-35 na tayari imechukua ndege tatu kuzifanyia majaribio.
Ndege ya F-35Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNdege ya F-35
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment