MAMBO SI SHWARI TENA AFRIKA YA KUSINI..Wageni wajihami Afrika Kusini na kujilinda wasiuawe na wenyeji..


Makundi ya wahamiaji waliiojihami nchini Afrika KusiniHaki miliki ya pichaEPA
Image captionMakundi ya wahamiaji waliiojihami nchini Afrika Kusini
Raia wa Kisomali wamejihami dhidi ya uvamizi wowote wa Wageni mjini Pretoria katika eneo la Marastabad nchini Afrika Kusini.
Kundi hilo lilikuwa linakabiliana na kundi jingine la raia wa Afrika kusini wanaoongoza ghasia dhidi ya wahamiaji.
Hatahivyo maafisa wa polisi waliingilia kati na kuwatimua kwa kutumia ndege aina ya helikopta pamoja na risasi za mipira.
Makundi ya wahamiaji nchini Afrika KusiniHaki miliki ya pichaEPA
Image captionMakundi ya wahamiaji nchini Afrika Kusini
Takriban watu wawili wamejeruhiwa na risasi hizo za mipira wakati polisi walipokuwa wakitawanya maandamano dhidi ya wageni nchini humo.
Mpiga picha mmoja alipigwa risasi mbili za mipira mgongoni alipokuwa akirudi nyumbani kutoka shule.
Maafisa wa polisi wametumia ndege aina ya helikopta ,risasi za mipira na vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji hao kuzuia makundi ya wahamiaji yaliojitokeza yaliojihami na fimbo,mawe na visu.
Wanaharakti wa shirika la Save South Afrika wanasema kuwa Meya wa Johannesburg Herman Mashaba ana maswali mengi ya kujibu.
Maafisa wa polisi wawatawanya waandamanaji Afrika KusiniHaki miliki ya pichaEPA
Image captionMaafisa wa polisi wawatawanya waandamanaji Afrika Kusini
Licha ya Bwana Mashaba kusema kuwa ghasia hizo hazina nafasi katika taifa hil,o wanaharakati wa shirika hilo wanadai kuwa matamshi yake kwamba wahamiaji nchini humo ndio wanaohusishwa na uhalifu ndio yaliosababisha ghasia hizo.
bbc
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment