Magari yapigwa marufuku Mogadishu kabla ya uchaguzi wa Rais.


Barabara za Mogadishu mara nyingi zina magari mengiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBarabara za Mogadishu mara nyingi zina magari mengi
Marufuku ya magari imetangazwa kwenye barabara kuu za mjini Mogadishu nchini Somalia, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa urais kesho Jumatano.
Waandishi wa habari wanasema kuwa shule nyingi na maofisi yamesalia yamefunguliwa lakini watu walilazimika kutembea ili kufika maeneo yao.
Wabunge watakusanyika kwenye uwanja wa ndege siku ya Jumatano kumchagua rais mpya,.
Kumekuwa na hofu kuwa kundi la wanamgambo la al-Shabab ambalo limeendesha mashambulizi mengi mjini Mogadishu, huenda likavuruga uchaguzi huo.
Uwanja wa ndege unaonekana kama eneo salama zaidi kwenye mji mkuu wa Mogadishu na uchaguzi ulihamishiwa huko kutoka kwa taasisi ya polisi kutokana na wasi wasi wa kiusalama.
Hatua za kiusalama za siku ya Jumatano zinahusu marufuku kwa safari za ndege kutoka uwanja wa Mogadishu.
Zaidi ya wagombea 20 wanawania wadhifa wa Rais. Rais wa sasa Hassan Sheikh Mohamud, anawania tena na wadadisi wanasema kuwa ni mmoja wa wale watakaosonga mbele kuwania katika duru zingine,
BBC
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment