Je nani ni muuaji wa Kim Jong Nam ?


Korea ya Kaskazini
Image captionKim Jong Nam, marehemu kwa sasa
Aliyekuwa ndugu wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, inaarifiwa kuwa chanzo cha kifo chake ni mauaji dhahiri yaliyotokea katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur nchini Malaysia.
Nao polisi nchini Malysia wamesema kwamba Kim Jong Nam alishambuliwa siku ya Jumatatu wakati alipokuwa akitarajia kuabiri kuelekea Macao.Kabla hajafariki dunia wakati akipelekwa hospitalini, alitoa maelezo kuwa alivutwa kutoka kwa nyuma na kumwagiwa kimiminika usoni mwake.
Uchunguzi wa kitabibu utafanywa ili kuweza kubaini chanzo cha kifo, huku kukiwa na tetesi kuwa huenda kimiminika alichomwagiwa usoni huenda ikawa ni simu.
Chanzo kutoka katika serikali ya Marekani kinasema kwamba wanaamini kwa dhati kuwa bwana Kim, aliyekuwa anaishi uhamishoni ameuawa na mawakala kutoka Korea Kaskazini.
BBC
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment