Donald Trump amponda mtangulizi wake


Marekani
Image captionRais wa Marekani Donald Trump
Rais Donald Trump ametumia mkutano wake na waandishi wa habari uliopangwa ghafla na ikulu ya Marekani kudai kuwa amerithi matatizo, ndani ya Marekani na nje.
Amewaambia waandishi wa habari kuwa, ajira zinakwenda nje ya Marekani na kwamba chama cha Demokrat kimeharibu mambo, lakini akaongeza kusema kuwa serikali yake inafanya kazi kama mashine kurekebisha hali hiyo.
Rais Trump pia ameendeleza vita vyake dhidi ya vyombo vya habari, ambazo amevituhumu kwa kutoa taarifa za uwongo. Bwana Trump pia amesema nakala mpya iliyopitiwa inayohusu marufuku yake ya kusafiri ambayo imezuiliwa na mahakama, itachapishwa wiki ijayo.
Amesema utekelezaji wake ulikuwa mzuri, lakini uamuzi wa mahakama ndio ulivuruga.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment