DC TUNDURU ASHIRIKI ZOEZI LA UOKOAJI WA WACHIMBAJI MADINI KATA YA MUHUWESI, MCHIMBAJI MMOJA AFARIKI BAADA YA KUANGUKIWA NA JIWE


Na Steven Augustino, Tunduru
Pichani (kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera (aliyevaa koti) akishuhudia uokoaji wa wachimbaji walioangukiwa na jiwe. Picha (kulia) Afisa Madini Wilaya ya Tunduru Fredrick Mwanjisi akimsaidia mchimbaji Rashidi Molina baada ya kunasuliwa katika jiwe lililowaangukia yeye na wenzake wawili.

MTU mmoja amefariki dunia katika ajali ya kuangukiwa na mawe katika machimbo ya madini ya vito yaliyipo katika Kijiji cha Muhuwesi Wilayani Tunduru mkoni Ruvuma.


Sambamba na tukio la kifo hicho pia watu wawili wameripotiwa kujeruhiwa na kutokana na kubanwa na mawe yaliyo poromoka katika shimo ambalo walikuwa wanachimba.

Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Wilaya hiyo Juma homera ambaye alishiriki katika tukio la uokoaji wa watu hao alisema kuwa tukio hilo lilitpkea February 19 majira ya saa 6. Mchana wakati watua hao wakiendelea shughuli za uchimbaji katika eneo la mto muhuwesi.
 
Rashidi Molina, akibebwa na wananchi waliokuja kuwasaidia, baada ya kunasuliwa kutoka katika jiwe lililowabana yeye na wenzake.
Aidha Dc, Homera aliwaja  walikubwa na mkasa huo kuwa ni Kanje Ally Kanje Mkazi wa Kijiji cha Ausilinda mjini hapa ambaye alifariki dunia katika eneo la tukio hilo.

Kwa mujibu wa Dc, Homera waliojeruhiwa ni Rashid Hasan Molida (25) ambaye alikuwa anachimba madini hayo pamoja na marehemu na Gerson Gerion (26) msaidizi wa kuendesha mtambo uliotumika kuokolea ambaye alibanwa na jiwe mojawapo wakati akiwa katika shughuli hiyo.

Alisema kilicho sababisha  watu hao kupatwa na madhara hayo ni ukaidi wa maelekezo ya serikali kupitia wataalamu wa idara ma yadini mabo kwa sasa walikuwa wamesitisha zoezi la uchimbaji wa madini katika eneo hilo kwavile siyo salama.
 
Rashidi Molina akiwa amenasa katikati ya mawe baada ya kuangukiwa, walipokuwa wakichimba madini ya vito, kandokando mwa mto Muhuwesi.
Alisema eneo hilo lina miamba mikubwa ambayo inahitaji wachimbaji wake wake na vifaa vyenye uwezo mkubwa wa kuyaondoa mawe yaliyopo katika eneo hilo na kufanya shughuli zao kwa usalama.

Akizungumzia tukio hilo afisa madizi mkazi wa wilaya ya Tunduru Fredrick Mwanjisi alisema kuwa tayali ofisi yake ilikwisha toa zuwio kwa wachimbaji kuendelea na shughuli hizo kutokana na eneo hilo kuwa na ugongo na mawe ambayo huanguka wakati wa mvua.
Alisema lakini kutokana na ubishi wa kutofuata maelekezo ya wataalamu watu hao walienda katika eneo hilo na kuchimba kwa njia ya wizi huku wakiwa hawana leseni jambo ambalo limepelekea kifo kwa mtu huyo na wengine kupata vilema vya maisha.


Alisema baada ya kukamilika kwa zoezi la uokoaji shimo hilo litafukiwa kwa kutumia mawe makubwa na kushindiliwa ili kuondoa hatari ya aina hiyo kwa watu wengine ambao walikuwa wanatamani kwenda kuchimba naada ya watu kuondoka.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Dkt. Alex Kazula alikiri kupokea mwili wa marehemu Kanje pamoja na majeruhi wawili waliopelekwa kupata matibabu katika hospitali ya serikali ya wilaya hiyo.

Alisema katika tukio hilo maafisa tabibu ambao alishirikiana nao katika utoaji wa huduma kwa majeruhi hao walibaini uwepo wa mivunjiko katika paja la mguu wa kulia wa Rashid Morina ambaye alidai kuwa wamepanga kumpeleka katika hospitali ya Misheni ya Ndanda yenye wataalamu wa mifupa kwa matibabu zaidi.

Kuhusu majeruhi Gerin, Dkt. Kazula alisema kuwa yeye alipata michubuko katika nyama za juu na kwamba atatibiwa katika hospitali hiyo na ataruhusiwa baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina.

Kuhusu taarifa za marehemu Kanje Dkt. Kazula alisema kuwa chanzo cha kifo chake kilisabaishwa na kupasuka kwa mabavu na viungi mbalimbali ndani ya mwili wake baada ya kubanwa na jiwe kubwa sehemu za kifuani.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Zubery Mwombeji amedhibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kwamba polisi wanendelea kufanya uchunguzi wa chanzo chake.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment