Wanajeshi wadhibiti mji kaskazini mwa Ivory Coast


Waasi wa Forces NouvellesImage copyrightAFP/GETTY
Image captionWaasi wa Forces Nouvelles walidhibiti maeneo ya kaskazini mwa Ivory Coast kati ya 2002 na 2011

Wanajeshi wadhibiti mji kaskazini mwa Ivory Coast

Wanajeshi ambao hawajaridhishwa na serikali wamevamia vituo va polisi katika mji wa Bouake nchini Ivory Coast, vyombo vya habari vimeripoti.
Taarifa zinasema wanajeshi hao wamedhibiti mji huo wa pili kwa ukubwa nchini humo.
Meya wa Bouake ameambia BBC kwamba mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mzozo huo yanaendelea.
Kumetokea pia ufyatuaji wa risasi katika mji wa Daloa, magharibi mwa Bouake.
Baadhi ya taarifa zinasema wanajeshi hao wanalalamikia kutolipwa marupurupu.
Shirika la habari la Reuters, likinukuu mwanahabari na afisa wa jeshi mjini Bouake, limesema mapigano yalianza mwendo wa saa nane usiku na mji huo sasa unadhibitiwa na wanajeshi wa zamani.
Gazeti la Abidjan Press limeripoti kwamba wanajeshi walichukua udhibiti wa barabara mbili mjini humo na walikuwa wamemshika mateka afisa mkuu mmoja wa jeshi kwa muda.
Shirika la habari la AFP limemnukuu mwanajeshi mmoja akisema waliochukua silaha ni "wapiganaji wa zamani walioingizwa kwenye jeshi ambao wanadai bonasi ya CFA 5m ($8,000) kila mmoja pamoja na nyumba".
Bouake
Mji mkuu wa Bouake ulikuwa ngome ya waasi waliodhibiti nusu ya taifa hilo upande wa kaskazini kuanzia 2002 hadi wakati wa kuunganishwa tena kwa taifa hilo baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2011.
Afisa wa jeshi Abidjan amesema wanajeshi zaidi wametumwa Bouake.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment