Trump amteua jaji wa mahakama kuu Neil Gorsuch


Rais Donald Trump amemteua Neil Gorsuch kuwa jaji wa mahakama kuu
Image captionRais Donald Trump amemteua Neil Gorsuch kuwa jaji wa mahakama kuu
Rais Donald Trump amemteua Neil Gorsuch kujaza nafasi katika mahakama kuu kwa mwaka mmoja .
Bw Gorsuch mwenye umri wa miaka 49 ni jaji katika mahakama ya rufaa mjini Denver.
Jaji huyo hatarajiwi kutoa hukumu juu ya utoaji mimba na ndoa za wapenzi wa jinsi moja.
Hata hivyo uteuzi wake unasubiri kuidhinishwa na bunge la Seneti.
Maseneta wa Democratic wametishia kumfungia nje mgombea yeyote atakayeonekana kuwa mhafidhina.
Waandamanaji wapinga uteuzi wa Neil Gorsuch kuwa jaji wa mahakama ya juu
Image captionWaandamanaji wapinga uteuzi wa Neil Gorsuch kuwa jaji wa mahakama ya juu
Awali maseneta hao walipinga uteuzi wa watu watatu uliofanywa na rais kuchukua wadhifa wa waziri.
Walisusia vikao vya kuwaidhinisha mawaziri wa fedha na afya waliopendekezwa na kuchelewesha upigaji kura wa kumuidhinisha Jeff Sessions aliyeteuliwa kuwa Mwanasheria mkuu.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment