Siku chake baada ya kuondoka nchini kwake Gmabia..Kamanda wa Jammeh akamatwa Senegal


Yahya JammehHaki miliki ya pichaAFP
Image captionYahya Jammeh
Vikosi vya nchi za Afrika Magharibi vimemkamata kamanda mmoja wa cheo cha juu nchini Gambia, na kupata silaha kweye makao ya kibinafsi ya rais wa zamani aliye uhamishoni Yahya Jammeh.
Jenerali Bora Colley, mkuu wa kikosi maalum alikamatwa katika nchi jirani ya Senegal.
Vikosi vya kikanda pia vimevamia nyumba ya bwana Jammeh iliyo kijiji mwao eneo la Kanilai na kupata silaha.
Jenerai Colley alikuwa kamanda wa zamani wa kambi ya jeshi ya Kanilai ambapo Jammeh alikuwa na mpango wa kahamia akistaafu, kabla ya kulazimishwa kukimbilia uhamishoni kwa kukataa kushindwa kwenye uchaguzi wa Disemba mosi mwaka 2016.
Walinzi wanne wa mke wa Jammeh, Zainab, pia nao walikamatwa kwenye mji wa mpaka wa Karang nchini Senegal.
Vikosi vya kikada vimekuwa vikimsadia Rais Adama Barrow kuchukua hatamu za uongozi, katika taifa hilo dogo la Afrika Magharibi tangu bwana Jammeh akimbilie uhamishoni zaidi ya wiki moja iliyopita.
BBC
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment