Rais wa Gambia asema hatong'atuka mamlakani


Rais Yahyah Jammeh wa Gambia
Image captionRais Yahyah Jammeh wa Gambia
Rais wa Gambia Yahya Jammeh amesema kuwa hatojiuzulu kabla ya uamuzi wa mahakama ya juu kuhusu utata uliogbikwa uchaguzi mkuu, uamuzi ambao huenda ukatolewa mwezi Mei.
Katika hotuba yake katika runinga ya kitaifa ,kiongozi huyo ambaye amekuwa mamlakani kwa kpindi kirefu pia amesisitiza matamshi yake ya hapo awali ya kushtumu mataifa ya kigeni kwa kuingilia siasa za taifa hilo.
Wapatanishi kutoka eneo hilo wakiongozwa na Nigeria wanatarajiwa nchini Gambia siku ya Ijumaa ili kumshinikiza kukubali kushindwa kufuatia uchaguzi huo wa mwezi Disemba.
Rais mteule Adama Barrow amesema kuwa ataapishwa wiki ijayo.
Bwana Jammeh ambaye awali alikuwa amekubali kushindwa katika uchaguzi huo, aliwasilisha kesi mahakamani baada ya tume ya uchaguzi kubadilisha baadhi ya matokeo.
Lakini tume hiyo inasisitiza kuwa matokeo hayo hayakuathiriwa na kwamba mfanyibiashara huyo alishinda kwa kura chache.
Bwana Jammeh alichukua mamlaka katika taifa hilo dogo mwaka 1994 na ameshtumiwa kwa unyanyasaji wa haki za kibinaadamu ijapokuwa ameshiriki katika uchaguzi kadhaa.
BBC
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment