NYASA WAZINDUA RASMI VIVUTIO MBALIMBALI VYA UTALII


Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge akiwa katika boti ya kisasa inayotumiwa na idara ya maliasili na uvuvi wilaya ya Nyasa kabla ya kuzunguka ziwa Nyasa kuangalia vivutio mbalimbali vya utalii katika wilaya ya Nyasa mkoani humo,kushoto ni mkuu wa wilaya ya Nyasa Esabila Chilumba.
Naibu waziri wa elimu na mafunzo mhandisi Stella Manyanya kushoto akimsikiliza askofu wa kanisa la Anglikana Doyasisi ya Ruvuma Raphael Reuben Haule ndani ya boti la Mv Matema linalofanya safari zake kati ya kijiji cha Liuli na maeneo mengine ndani ya ziwa Nyasa,katikati mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge katikati akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Tamasha la kuvitangaza vivuutio vya utalii katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma jana,kulia mkuu wa wilaya ya Mbinga Kosmas Nshenye,wa pili kulia mkuu wa wilaya ya Nyasa Esabila Chilumba na kushoto nmbunge wa jimbo la Nyasa Stella Manyanya.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge akiangalia kahawa ya kopo inayolimwa katika wilaya ya Nyasa na kusindikwa katika kiwanda cha kukoboa kahawa cha Mbinga ambayo ni moja kati ya rasimali na utajiri uliopo katika wilaya Nyasa,kulia ni mkuu wa wilaya ya Nyasa Esabela Chilumba na kushoto Mbunge wa jimbo la Nyaa na naibu waziri wa elimu Stella Manyanya.
Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Nysasa mkoani Ruvuma mhandisi Stella Manyanya kulia na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mafia mkoani Pwani Erick Mapunda wakiangalia makapu yanayotumika kubebea dagaa katika ziwa nyasa wakati wa Tamasha la kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika wilaya ya Nyasa.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge akizungumza jana na wananchi, watendaji wa serikali na wageni kutoka nje ya mkoa huo(hawapo pichani) waliofika katika uzinduzi wa Tamasha la kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika wilaya ya nyasa mkoani humo,kulia ni mkuu wa wilaya ya Nyasa Esabila Chilumba na kushoto mbunge wa jimbo la Nyasa ambaye pia ni naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Mhandis Stella Manyanya.
Nahodha wa boti ya kisasa iliyonunuliwana serikali kwa ajili ya kufanya kazi ya doria ya uvuvi haramu na kusaidia shughuli ya uokoaji katika ziwa nyasa Baraka Mguhi akimsaidia kuvaa jakti maalum(life jacket)mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge kabla ya kuzunguka ziwa nyasa kuangalia vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo katika wilaya ya Nyasa.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment