Nana Akufo-Addo ndiye rais mpya Ghana


Nana Akufo-Addo akila kiapo wakati akiapishwaImage copyrightREUTERS
Image captionNana Akufo-Addo akila kiapo wakati akiapishwa

Nana Akufo-Addo ndiye rais mpya Ghana

Wakili wa zamani wa haki za kibinaadamu, Nana Akufo-Addo, ameapishwa kuwa rais mpya wa Ghana, katika sherehe iliyohudhuriwa na viongozi kadha wa Afrika.
Katika hotuba yake ya kwanza, Nana Akufo-Addo, alimsifu rais anayeondoka madarakani, John Dramani Mahama, kwa namna alivokiri kushindwa katika uchaguzi wa mwezi uliopita.
Viongozi kadha wa Afrika walikusanyika katika mji mkuu wa Ghana, Accra, kuhudhuria sherehe za kutawazwa rais mpya, Nana Akufo Addo.
Maelfu ya wageni walialikwa kwenye sherehe katika Medani ya Uhuru mjini Accra.
Bwana Akufo Addo, aliyewahi kuwa wakili wa haki za kibinaadamu, alimshinda Rais John Dramani Mahama, katika uchaguzi wa mwezi uliopita.
Baada ya kuapishwa kwa rais, sasa viongozi waliohudhuria sherehe hiyo, watajadili namna ya kuhakikisha kuwa Rais wa Gambia, Yahya Jammeh, anaondoka madarakani.
Kiongozi huyo amekataa kustaafu ingawa alishindwa katika uchaguzi wa Mwezi Disemba.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment