MUHIMBILI YATEMBELEWA NA UJUMBE KUTOKA MAREKANI LEO


 Wageni hao wakiwamo wakurugenzi wa hospitali hiyo wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wakati akiwaeleza changamoto na mafanikio ya hospitali hiyo.  Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji katika hospitali hiyo, Dk Julieth Magandi, Anne Hussian, Cheryl Grasmoen kutoka Chuo Kikuu cha Mennisota, Marekani na Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi, Dk. Praxeda Ogweo wa Muhimbili.
 Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Juma Mfinanga akiueleza ujumbe huo kazi zinazofanywa na idara yake.
 Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali hiyo, Dk. Flora Lwakatare akizungumza na ujumbe huo leo.
 Profesa wa Masuala ya Utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Minnesota, Michelle Biros akiwa  na Mkuu wa Idara ya Mionzi wa Muhimbili, Dk. Flora Lwakatare wakati wakielekea katika chumba cha CT-Scan.
 Dk Lwakatare akitoa maelezo kwa ujumbe huo jinsi CT-scan inamvyofanya kazi. 
 Mmoja wa msimamizi wa wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu wa hospitali hiyo, Trustworthy Majuta akifafanua jambo wa ujumbe huo leo.
 Mkuu wa Idara ya Wagonjwa wa Nje, Dk Raymond Mwenesano akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe huo leo. Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Ujumbe wa watu watano kutoka Chuo Kikuu cha Tiba cha Minnesota kutoka nchini Marekani leo wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendajji wa hospitali hiyo, Profesa  Lawrence Museru.

Ujumbe huo umeongozwa  na Mkuu wa masuala ya utafiti  katika Idara ya Magonjwa ya dharura kutoka Chuo hicho,  Profesa Michelle Biros .

Katika mazungumzo hayo Profesa Museru ameuleza ujumbe huo mikakati na malengo mbalimbali ambayo MNH inafanya katika kuhakikisha huduma za kibingwa zinafanyika nchini ikiwa ni pamoja na upandikizaji wa figo, kuweka kifaa maalum cha usikivu  na kuongeza wodi kwa ajili ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum.

Kwa mujibu wa Profesa Museru, MNH inakabiliwa na changamoto ya wataalam  katika baadhi ya maeneo ikiwamo ICU.

Maeneo waliotembelea ni  Idara ya Magonjwa ya  dharura na Ajali, Idara ya Mionzi, Mwaisela -wodi moja, Jengo la watoto na Jengo la wazazi namba mbili -Wodi 35.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment