Maiti ya mfalme Kigeli yawasili Rwanda


Mfalme Kigeli amekuwa akiishi uhamishoni mjini Washington tangu mwaka 1992Haki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionMfalme Kigeli amekuwa akiishi uhamishoni mjini Washington tangu mwaka 1992
Maiti ya mfalme wa mwisho nchini Rwanda, Kigeli wa tano yawasili chini humo kufuatia kesi ya mahakaman kati ya familia yake, kuhusu ni wapi angezikwa.
Mfalme Kigeli ambaye amekuwa akiishi uhamishoni mjini Washington tangu mwaka 1992, aliaga dunia mwezi Oktoba akiwa na umri wa miaka 80.
Kifo chake kilizua mzozo ndani ya familia, kati ya ile inayoishi nchini Marekani na iliyo nchini Rwanda kuhusu ni wapi angezikwa kabla ya mahakama ya Marekanikutoa hukumu kuwa atazikwa nyumbani kwao.
Hata hivyo baraza la kifalme la mfalme Kigeli liliseme kwenye taarifa kuwa hakutaka kuzikwa nchini Rwana ikiwa serikali ya sasa ambayo ilipinga ufalme wake ilikuwa bado mamlakani.
Mfalme Kigeli aliingia madarakani mwaka 1959 na akalazimika kuihama nchi mwaka uliofuatia baada ya kukosana na koloni ya ubelgiji.
Mwaka 1961 ufalme huo ulivutwa na mfalme akaanza maisha ya kuishi uhamishoni Afrika Mashariki ikiwemo nchini Kenya na Uganda kabla ya kuhamia nchini Marekani.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment