Korea Kaskazini kutengeza kombora la masafa marefu


Rais KIm Jong Un wa Korea KaskaziniImage copyrightREUTERS
Image captionRais KIm Jong Un wa Korea Kaskazini

Korea Kaskazini kutengeza kombora la masafa marefu

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema kuwa taifa lake linakaribia awamu ya kutengeza kombora la masafara marefu ambalo lina uwezo wa kubeba bomu la nuklia.
Katika hotuba ya kuukaribisha mwaka mpya iliopeperushwa hewani katika runinga ya taifa Bw Kim amesema kuwa Korea Kaskazini imeimarika kama taifa lenye uwezo wa kinyuklia mwaka 2016.
Pyongyang imefanya majaribio mawili ya kombora la kinyuklia katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita ikiwa ni mojawapo ya majaribio yake makubwa kufikia sasa.
Hatua hiyo ilizua shutuma mbalimbali na kuvutia vikwazo vya kimataifa .
Haijulikani taifa hilo imekaribia kivipi kutengeza kombora la Kinyuklia ambalo linaweza kurushwa na kufika Marekani.


SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment