Kivuli cha Col Muammar Gadaff charudi Umoja wa afrika


Ramani ya Morocco
Image captionRamani ya Morocco

Kivuli cha Col Muammar Gadaff charudi Umoja wa afrika, 
Tangu AU impteze Col Gadaff imekuwa ikipita wakati mgumu kujiendesha na kutekeleza baadhi ya maazimio yanayohitaji kiasi kikubwa cha fedha, kwa sababu kwa wakati huo Libya ya Gadaff ilikuwa mchangiaji mkuu wa AU.

Kwa sasa nchi ya Morocco imerudi katika Umoja wa Afrika AU na inatajwa kuziba pengo la Col Gadaff kwa sababu Morocco ni moja ya mataifa ya kaskazini mwafrika yaliyopiga hatua kimaendeleo katika sekta mbali mbali kama Utalii, Kilimo, uwekezaji, na usafiri wa anga

Viongozi wa umoja wa Afrika wameamua kuirudisha Morocco katika shirika la Umoja wa Afrika AU zaidi ya miongo mitatu baada ya taifa hilo la ufalme wa Afrika Kaskazini kujiondoa katika AU kufuatia mgogoro wa eneo la Sahara magharibi.
Shirika hilo linatambui Sahara ya Magharibi kuwa jimbo huru, lakini Morrocco inasema kuwa eneo hilo ni mkoa wake wa kusini.
Morocco imepigania mpango wake wa kutaka kujiunga tena na Umoja wa Afrika mwaka uliopita.
Eneo la Sahara ya Magharibi linaendelea kuwa eneo tata ,lakini viongozi wengi wa Afrika walipiga kura kuikubali Morrocco kurudi katika Umoja wa Afrika.
BBC..
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment