Kituo kinachomkosoa Yahya Jammeh chafungwa Gambia


Kiongozi wa Gambia Yahya JammehImage copyrightREUTERS
Image captionKiongozi wa Gambia Yahya Jammeh

Kituo kinachomkosoa Yahya Jammeh chafungwa Gambia

Mamlaka nchini Gambia imekifunga kituo kimoja cha habari ambacho kimekuwa kikimkosoa rais wa taifa hilo Yahya Jammeh.
Maafisa wa Ujasusi waliagiza kituo cha habari cha Teranga FM kufungwa bila ya kutoa sababu ,alisema Emil Touray mkuu wa vyombo vya habari nchini humo.
Hii ni ishara ya kwanza ya vita dhidi ya vyombo vya habari tangu bwana Jammeh kukataa kushindwa katika uchaguzi wa Disemba mosi.
Bwana Jammeh alichukua mamlaka katika mapinduzi ya serikali mwaka 19194.
Awali alikuwa amekubali kushindwa na mfanyibiashara Adama Barrow, lakini akaenda mahakamani ili kupinga matokeo hayo,akisema uchaguzi hu ulikumbwa na udanganyifu.
Tume ya uchaguzi nchini humo imesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment