Khamenei na salamu za rambirambi, kifo cha Rafsanjani


Akbar Hashemi RafsanjaniImage copyrightAP
Image captionAkbar Hashemi Rafsanjani

Khamenei na salamu za rambirambi, kifo cha Akbar Hashemi Rafsanjani,

Kiongozi wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ameongoza kutoa salam za rambirambi za kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Akbar Hashemi Rafsanjani, aliyefariki dunia, akiwa na umri wa miaka themanini na mbili.
Licha ya tofauti walizokuwa nazo viongozi hao, lakini kiongozi huyo wa dini amemtaja Rafsanjani kama mpambanaji.
Rafsanjani alikuwa akimuunga mkono rais wa sasa Hassan Rouhani ambae amemsifu kuwa ni mwana mapinduzi mkubwa.
Siku tatu za maombolezi zimetangazwa.
Ayatollah Rafsanjani aliwahi kuwa rais kati ya mwaka 1989 hadi 1997 na ameendelea kuwa na nafasi muhimu katika siasa za Iran.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment