Haya ndio maajabu ya Wachimbaji mgodi 15 waliokwama ardhini kwa zaidi ya siku 5..ni muujiza wa Mungu pekee umewaokoa.

Wafanyakazi 15 wa mgodi waokolewa Tanzania

Image captionWafanyakazi 15 wa mgodi waokolewa Tanzania
Wachimbaji madini 15 wameokolewa wakiwa hai baada ya mgodi wao kupolomoka siku tatu zilizopita
Ajili hiyo iliyokea usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita, tarehe 26 Januari, katika mgodi uitwao RZ Gold Mine, unaomilikiwa na raia wa China katika machimbo ya dhahabu yaliyopo Geita Kaskazini Magharibi mwa Tanzania
Manusura hao ni raia 14 wa Tanzania na mmoja wa China.
Mwandishi wa BBC Halima Nyanza aliyeshuhudia zoezi la uokoaji anasema eneo hilo lilijawa na shangwe na vilio vya furaha wakati ndugu, jamaa na wachimbaji wengine walipokuwa wakishuhudia uokoaji wa manusura hao.
Wafanyakazi 15 wa mgodi waokolewa Tanzania
Image captionWafanyakazi 15 wa mgodi waokolewa Tanzania
Manusura hao walionokena wadhaifu kiafya, lakini walipatiwa huduma ya kwanza mara moja na kisha kupelekwa katika kituo cha afya kilichopo jirani
Uchunguzi wa nini hasa kilisababisha ajali hiyo unaendelea, lakini hii si mara ya kwanza kwa tukio kama hili kutokea
Mwaka jana mwezi Novemba, Tanzania ilisherehekea ukoaji wa 'kimiujiza' baada ya wachimbaji watano kuokelewa wakiwa hai baada ya kukwama chini ya ardhi kwa siku 41.
Eneo la Magharibi mwa Tanzania lina migodi mingi na wachimbaji wengi hutoka vijiji vya jirani.
Wafanyakazi 15 wa mgodi waokolewa Tanzania
Image captionWafanyakazi 15 wa mgodi waokolewa Tanzania
Hata hivyo migodi mingi haikaguliwi mara kwa mara na hali ya usalama ya migodi hii haitimizi viwango rasmi.
Naibu waziri wa nishati Dkt Medard Kalemani, amesema serikali itahakikisha wachimbaji wana kuwa salama.
Mgodi huo utakuwa chini ya uangalizi kwa siku tano kabla wachimbaji kuruhusiwa kufanya kazi.
Naibu waziri pia amewaagiza makamishina wa madini kufanyia tathmini migodi mwingine ya wachimbaji wadogo kwa siku tano, kuanzia kesho
Wafanyakazi 15 wa mgodi waokolewa Tanzania
Image captionWafanyakazi 15 wa mgodi waokolewa Tanzania
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment