Gambia: Yahya Jammeh apewa makataa ya mwisho


Kusherehekea Adama Barrow mjini Banjul, 19 Januari 2017Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionHabari za kuapishwa kwa Adama Barrow zilipokelewa kwa furaha na shangwe Banjul
Viongozi wa nchi za Afrika Magharibi wamempa Yahya Jammeh fursa ya mwisho kuachia madaraka, huku wanajeshi wa Senegal wakiingia nchini Gambia.
Bw Jammeh amepewa hadi saa sita mchana Ijumaa kuachia madaraka la sivyo aondolewe kwa nguvu na wanajeshi wa nchi za Afrika Magharibi wanaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
Wanajeshi hao wametakiwa kusubiri hadi makataa hayo yamalizike.
Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (Ecowas) inaunga mkono Adama Barrow, ambaye aliapishwa kuwa rais mpya wa Gambia katika ubalozi wa nchini hiyo nchini Senegal.
Juhudi za mwisho za kumshawishi Bw Jammeh kuondoka kwa hiari, ambazo zinaongozwa na Rais wa Guinea Alpha Conde, zinatarajiwa kufanyika Ijumaa asubuhi.
Mwenyekiti wa tume ya Ecowas, Marcel Alain de Souza, alisema iwapo mkutano huo utakaoongozwa na Bw Conde hautafaulu, basi hatua ya kijeshi itafuata.
"Iwapo kufikia saa sita mchana, yeye (Bw Jammeh) hatakubali kuondoka Gambia chini ya Rais Conde, tutaingilia kijeshi," amesema.
Adama BarrowHaki miliki ya pichaRTS
Image captionAdama Barrow baada ya kuapishwa aliwaamuru wanajeshi wa Gambia wasalie kambini
Wanajeshi wa Ecowas walisema hawakukumbana na pingamizi zozote kutoka kwa wanajeshi wa Gambia walipoingia nchini humo Alhamisi baada ya kuapishwa kwa Barrow.

Wanajeshi kutoka Senegal na nchi nyingine za Afrika Magharibi waliingia Gambia baada ya makataa mengine aliyopewa Bw Jammeh kuondoka kumalizika.
Bw Jammeh, ambaye bado yupo nchini Senegal amesema hatarejea mji mkuu wa Gambia, Banjul, hadi operesheni ya kijeshi imalizike.
Hatua ya Ecowas kutaka kumtoa kwa nguvu Jammeh inaungwa mkono na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye wanachama 15, ingawa baraza hilo lilisisitiza kwamba suluhu ya amani inafaa kupoewa kipaumbele.
SenegalHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWanajeshi wa Senegal ni miongoni mwa waliopokea mafunzo zaidi Afrika
Msemaji wa jeshi la Senegal Kanali Abdou Ndiaye, aliambia BBC kwamba wanajeshi wa Senegal tayari wamo nchini Gambia na wamejiandaa kupigana hali ikibidi.
"Tayari hivi ni vita, tukikumbana na upinzani wowote, tutapigana," amesema, na kuongeza: "Iwapo kuna watu wanampigania rais huyo wa zamani, tutapigana nao."
Lakini Kanali Ndiaye alisema lengo kuu la Ecowas ni kurejesha demokrasia na kumruhusu rais huyo mpya kuchukua hatamu.
Kwenye hotuba yake baada ya kuapishwa mjini Dakar, Rais Barrow aliwaamuru wanajeshi wanajeshi kusalia kambini.
Alisema wanajeshi watakaopatikana wakiwa na silaha nje ya kambi watachukuliwa kuwa "waasi."

Mbona Jammeh hataki kuondoka madarakani?
Jammeh anataka uchaguzi mpya ufanyike GambiaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJammeh anataka uchaguzi mpya ufanyike Gambia
Bw Jammeh awali alikubali kwamba Bw Barrow alishinda uchaguzi lakini baadaye akabadili msimamo wake na kusema hangeachia madaraka.
Alitangaza hali ya tahadhari ya siku 90 na kuhimiza "amani, utulivu na kufuatwa kwa sheria" baada ya kile alichosema ni udanganyifu uchaguzini.
Alisema tume ya uchaguzi ilifanya makosa mengi, na baadhi ya wafuasi wake walizuiwa kupiga kura vituoni.
Tume hiyo baadaye ilikubali kwamba baadhi ya matokeo yaliyotangazwa yalikuwa na makosa, lakini ikasema makosa hayo hayangeathiri ushindi wa Bw Barrow.
Bw Jammeh amesema atasalia madarakani hadi uchaguzi mpya ufanyike.
Hatua yake ya kuendelea kung'ang'ania madaraka itahakikisha kwamba hashtakiwi kutokana na makosa aliyoyatenda wakati wa utawala wake.
Mbona Senegal inaongoza kumkabili
Ecowas, Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, iliipa Senegal jukumu hilo kwa sababu taifa hilo linaizunguka Gambia.
Kanali Abdou Ndiaye, msemaji wa jeshi la Senegal, amesema Ecowas iliamua kumuwekea Jammeh makataa ili kujaribu kupata suluhu ya kidiplomasia.
Map of The Gambia
Wanajeshi wote wa Gambia ni takriban 2,500.
Hii inaifanya vigumu kufikiria ni vipi wanaweza kuwashinda wanajeshi wa kanda hiyo, anasema mwandishi wa BBC wa masuala ya usalama Afrika Tomi Oladipo.
Nigeria imetuma ndege za kivita na ndege nyingine za kawaida, pamoja na wanajeshi 200 nchini Senegal. Wanajeshi hao walienda Senegal Jumatano asubuhi.
Meli za kivita za Nigeria pia zimewekwa tayari baharini.
Manowari moja iliondoka Lagos Jumanne na itakuwa na jukumu la kuwaokoa raia wa Nigeria walio nchini Gambia.
Ghana pia inachangia wanajeshi.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment