Jeshi la Syria lasema mapigano yapo katika hatua za mwisho Aleppo


Vikosi vya serikali vimefanikiwa kudhibiti eneo muhimu la Sheikh Saeed
Image captionVikosi vya serikali vimefanikiwa kudhibiti eneo muhimu la Sheikh Saeed

Jeshi la Syria lasema mapigano yapo katika hatua za mwisho Aleppo

Jeshi la Syria limesema mapigano ya mjini Aleppo yapo katika hatua za mwisho baada ya kufanikiwa kudhibiti sehemu kubwa ya mji huo kutoka mikononi mwa waasi.

Mkuu wa kamati ya usalama Luteni Jenerali Zaid al-Saleh, amesema wapiganaji waasi hawakuwa na muda walitakiwa kusalimu amri au kufa.
Maelfu ya raia wanaaminika kuzungukwa na waasi, ambapo maji na chakula vimekwisha.
Vikosi vya serikali pia vilidhibiti eneo la Saliheen siku ya Jumatatu
Image captionVikosi vya serikali pia vilidhibiti eneo la Saliheen siku ya Jumatatu
Kwa sasa waasi wamepoteza zaidi ya asilimia 90 ya udhibiti waliokuwa nao mashariki mwa Aleppo tangu serikali ilipoanzisha operesheni mwezi uliopita kuhakikisha inaudhibiti kabisa mji huo kutoka kwa waasi.
Urusi, inayounga mkono serikali, imesema zaidi ya raia 100,000 wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano na wapiganaji waasi 2,200 wamesalimu amri.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment