Don King, Mayweather wampa ‘ndondo’ meneja wa Cheka za kuandaa mapambano ya ngumi za kulipwa


Don King, Mayweather wampa ‘ndondo’ meneja wa Cheka za kuandaa mapambano ya ngumi za kulipwa

Promota na meneja wa bondia Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na bondia nyota na tajiri duniani, Floyd Mayweather Jr wakati wa mkutano mkuu wa 54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) unaoendelea kwenye ukumbi wa Hollywood Marekani.
Promota na meneja wa bondia Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na promota nyota dunaini, Don King wakati wa mkutano mkuu wa 54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) unaoendelea kwenye ukumbi wa Hollywood Marekani.
Promota na meneja wa bondia Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na bondia nyota Wladimir Klitschko wakati wa mkutano mkuu wa 54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) unaoendelea kwenye ukumbi wa Hollywood Marekani.
Promota na meneja wa bondia Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa mkuu wa 54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) unaoendelea kwenye ukumbi wa Hollywood Marekani.
Promota na meneja wa bondia Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na mtoto wa bondia nyota marehemu Mohammed Ali wakati wa mkutano mkuu wa 54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) unaoendelea kwenye ukumbi wa Hollywood Marekani.
Promota na meneja wa bondia Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na bondia nyota mtaafu, Evander Holyfied wakati wa mkutano mkuu wa 54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) unaoendelea kwenye ukumbi wa Hollywood Marekani.Meneja wa mabondia nyota nchini, Francis na Cosmas Cheka, Juma Ndambile amesema amejifunza na anaendelea kujifunza masuala mbalimbali ya kuendeleza mchezo wa ngumi za kulipwa duniani kupitia kwa mapromota wakubwa kama Don King.


Ndambile kwa sasa yopo nchini Marekani akihudhuria mkutano wa 54 wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) ulioanza jana kwenye ukumbi maalrufu wa Hollywood. Akiwa Mtanzania pekee katika mkutano huo, Ndambile alisema kuwa ameweza kujiunganusha na mapromota nyota duniani ili kuleta maendeleo katika mchezo huo hapa nchini.

Alisema kuwa ameweza kujadiliana na mapromota kadhaa ambao wanajua umuhimu wa mchezo wa ngumi za kulipwa na kupitia kampuni yake ya Advanced Security Limited ataweza kuandaa mapambano ya ngumi ya Kimataifa, yenye ubora wa hali ya juu.

“Ubora huo utatokana na mbinu za kutafuta masoko ya ‘kuuza’ pambano au mapambano ya ngumi, mchezo wa ngumi unapendwa sana, hivyo nikiwa Mtanzania pekee niliyepata fursa hiyo, nitaitumia ipasavyo ili kufikia malengo niliyojiwekea na kwa faida ya Tanzania,” alisema Ndambile kwa njia ya simu.

Alisema kuwa ameweza kupata ‘contact’ za mabondia makubwa, lengo kuu ni kuongeza wigo wa kazi zake na kufikia hatua ya juu kabisa katika ngumi za kulipwa.“Kinchotakiwa hapa ni kuwa makini na ‘serious’ katika kazi, ukichukulia mchezo wa ngumi kimchez mchezo, hautafikia mbali, lakini ukiuchukulia kama kazi na lengo ni kuendeleza vipaji na kujiongezea kipato, utafaidika wewe na mabondia wao,” alisema.

Mbali ya Dong King, Ndambile alikutana uso kwa uso na mabondia nyota kama Floyd Mayweather, Amir Khan, Wladimir Klitschko, Evander Holyfield, Lennox Lewis, Mike Tyson, Amir Khan na wengine wengi.

Alisema kuwa umoja ni selaha pekee ya kuendeleza mchezo wa ngumi hapa nchini. “Tofauti na wenzetu, hapa kwetu ni chuki, unafiki na mizengwe kibao, wenzetu wanashirikiana, lengo ni ‘kuuza’ mchezo na si vinginevyo, mtu akiandaa pambano, wanashirikiana wote,” alisema.

Mkutano huo umeshirikisha wadau wa ngumi za kulipwa zaidi ya 1000, unatarajia kumalizika Desemba 17. Mbali ya kutoa tuzo kwa mabondia na majadiliano kadhaa, mkutano huo pia ulimuenzi bondia nyota, marehemu, Mohamed Ali ambapo wadau wote walipiga picha kwenye sanamu yake.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment