Assad asema ushindi Aleppo ni muhimu


Rais Assad amesema ushindi wa vita vya Aleppo itakuwa muhimu kwaoImage copyrightAFP
Image captionRais Assad amesema ushindi wa vita vya Aleppo itakuwa muhimu kwao
Rais Bashar al-Assad amesema kuwa ushindi wa wanajeshi wake katika mapigano mjini Aleppo utakuwa ni hatua muhimu katika kumaliza mapigano nchini Syria.
Vikosi vyake pamoja na washirika wake,wameleta mabadiliko makubwa mjini humo na kuwekwa katika nafasi ya kuangamiza vikosi vya waasi vilivyosalia katika eneo hilo.
Awali katika hali isiyo ya kawaida viongozi wa nchi za magharibi, Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani waliamuru kusitishwa kwa mapigano hayo.
Wameeleza kuwa matatizo ya kibinadamu wanayoshuhudia pamoja na picha za watoto waliofariki zina vunja moyo.
Wameishutumu serikali ya Syria na muungano wao na Urusi kwa kile kilicho elezwa kuwa kikwazo kwa jitihada za misaada ya kibinadamu.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment