Wakuu wa wanahabari wafungwa Misri


Wakuu hao walifungwa kwa kuwapa hifadhi wenzao waliokuwa wakisakwa na polisi.
Image captionWakuu hao walifungwa kwa kuwapa hifadhi wenzao waliokuwa wakisakwa na polisi.
Kiongozi wa chama cha waandishi wa habari nchini Misri, na wakuu wengine wawili, wamehukumiwa kifungo cha miaka miwili, kwa kuwapa hifadhi wenzao waliokuwa wakisakwa na polisi.
Hukumu hiyo, ambayo inaweza kufutwa wakilipa faini ya dola miasita, inafuatia msako wa polisi kwenye ofisi ya jumuiya ya wafanyakazi mjini Cairo mwezi wa Mei, wakati polisi wakiwasaka waandishi wa habari wawili.
Hao walishutumiwa kulalamika juu ya uamuzi wa serikali ya Misri, kuikabidhi Saudi Arabia, visiwa viwili katika Bahari ya Sham.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment