RC MAKONDA AWATAKA WATENDAJI WOTE WA KATA KUWA NA TAARIFA ZOTE ZA MIRADI YA MAENDELEO


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na wananchi wa Kata ya Msigani mtaa wa Temboni juu ya watendaji wote wa Kata kuwa na taarifa zote za miradi ya maendeleo vinginevyo atawachukulia hatua stahiki leo jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimsikila Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Humphrey Polepole  alipokuwa akitolea ufafanuzi kuhusu mradi wa maji huo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikangua mradi wa maji ambao ulikuwa ukiratibiwa na kamati ya maji ya Mtaa ambapo ulionesha mapungufu na kwasasa mradi huo unasimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka DAWASCO
Mkazi wa Mtaa wa Temboni, Moroen Goube akifafanua jambo katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
Wananchi wa Mtaa wa Temboni wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo jijini Dar es Salaam.

Ikiwa ni muendelezo wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambapo leo ni siku ya nane tangu aanze ziara hiyo, akiwa katika ziara yake ndani ya Wilaya ya Ubungo Kata ya Msigani mtaa wa Temboni RC Makonda ametoa agizo kwa Watendaji Kata wote katika Mkoa wake.

RC Makonda amewataka watendaji wote wa Kata kuwa na taarifa zote za miradi ya maendeleo vinginevyo atawachukulia hatua stahiki.
"Sitaki Kumkuta Mtendaji yeyote wa Kata ambaye hajui jambo lolote kwenye kata yake" Alisema RC Makonda. 

Ambapo amemtolea mfano mzuri Mkuu wa Wilaya hiyo Humphrey Polepole kwa kuwa na taarifa mbalimbali kuhusu miradi ya maendeo na kuwaomba waige kutoka kwake.

Pia RC Makonda amemuagiza RPC Mkoa wa kipolisi Kinondoni Suzan Kaganda kwa kushirikiana na TAKUKURU kumshikilia na kumfanyia uchunguzi aliyekuwa Mtendaji wa Kata hiyo Neema Kalumbe ambaye kwa sasa ni Mtendaji wa Kata ya Makongo kujibu tuhuma za ubadhirifu wa fedha za mradi wa Barabara ya kutokea Msuguri na Msingwa ambao ulitengewa milioni 17 na hakuna barabara iliyojengwa. 

Katika hatua nyingine RC Makonda amemtaka mwenyekiti wa wa Mtaa huo wa Msigani Israel Mushi kutofanya kazi kwa upendeleo kwani kuna Mkazi aliyefahamika kwa jina la Maureen Gomba ambaye amelalamikia kuwa mwenyekiti huyo amekuwa akigawa vizimba kwa watu anaowafahamu. 

RC Makonda amewatoa hofu wakazi hao kuhusu huduma ya maji na kwani kwasasa mradi huo upo chini ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka DAWASCO, huku Mkuu wa Wilaya hiyo akihaidi kukutana na wananchi hao ili kumaliza kero hiyo kabisa ifikapo Desemba 21.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment