Mji wa kale wa zaidi ya miaka 7,000 wagunduliwa Misri

Luxor

Mji wa kale wa zaidi ya miaka 7,000 wagunduliwa Misri

Wanaakiolojia nchini Misri wamegundua kile wanachosema ni mabaki ya mji ambao ulikuwepo zaidi ya miaka 7,000 iliyopita.
Wamepata nyumba, vifaa, vyungu na makaburi makubwa.
Mabaki hayo yamo eneo la ukingo wa mto Nile, karibu na hekalu la Seti, eneo la Abydos.
Inaaminika kwamba maafisa wakuu na wajenzi wa makaburi, ambao huenda walihusika katika kujenga makaburi ya kifalme katika mji mtakatifu wa Abydos hapo karibu waliishi eneo hilo. Mji wa ABydos una mahekalu, na unaaminika kutumiwa kama mji mkuu wakati mmoja enzi za kale za utawala wa Misri.
Ramani

Wataalamu wanasema makaburi 15 yaliyogunduliwa yanaashiria kwamba ni watu wa hadhi ya juu waliozikwa humo.
Inaaminika kwamba mji huo ulikuwa makao ya maafisa wakuu wa serikali na wachimbaji na wajenzi wa makaburi, ambao ulifana enzi za kwanza kabisa za Misri ya kale.
Wataalamu wanasema ugunduzi huo huenda ukasaidia kufufua sekta ya utalii nchini humo ambayo imeathirika pakubwa kutokana na machafuko yaliyofuatia kuondolewa madarakani kwa Rais Hosni Mubarak mwaka 2011.
Mabaki ya mwili uliohifadhiwa ambao unakadiriwa kuwa wa zaidi ya milenia moja iliyopita yaligunduliwa na wanaakiolojia wa Uhispania karibu na Luxor mapema mwezi huuImage copyrightAFP
Image captionMabaki ya mwili uliohifadhiwa ambao unakadiriwa kuwa wa zaidi ya milenia moja iliyopita yaligunduliwa na wanaakiolojia wa Uhispania karibu na Luxor mapema mwezi huu
LuxorImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionMaeneo ya akiolojia karibu na Luxor (pichani) na kwingineko Misri yametatizika kuwavutia watalii kutokana na misukosuko ya kisiasa
Wanaakiolojia wanasema wamegundua vitu vingi kwenye mji huo vikiwemo majumba, vigae vya vyungu na vifaa vilivyoundwa kwa kutumia chuma na mawe.
Lakini mtathmini wa BBC wa masuala ya Mashariki ya Kati Alan Johnston anasema muhimu zaidi ni makaburi yaliyogunduliwa.
Inaaminika kwamba maafisa wakuu na wajenzi wa makaburi, ambao huenda walihusika katika kujenga makaburi ya kifalme katika mji mtakatifu wa Abydos hapo karibu waliishi eneo hilo. Mji wa ABydos una mahekalu, na unaaminika kutumiwa kama mji mkuu wakati mmoja enzi za kale za utawala wa Misri.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment