Mfalme mteule wa Thailand kuthibitishwa Desemba mosi


Mwana mfalme Vajiralongkorn
Image captionMwana mfalme Vajiralongkorn
BBC imetaarifiwa kwamba mfalme mteule mtarajiwa wa Thailand Vajiralongkorn atathibitishwa rasmi kama mfalme ajaye mnamo Desemba mosi.
Mwana wa mfalme huyo ambaye pia ni mfalme mtarajiwa alitarajiwa kupakwa mafuta na kutawazwa katika kipindi ama baada ya maziko ya babake , mfalme King Bhumibol Adulyadej, aliyefariki wiki tatu zilizopita, kutokana na yeye mwenyewe kuomba muda wa kumuomboleza babake.
Vajiralongkorn ana mtoto mmoja wa kiume aliyempata na mke wake wa zamani Srirasmi
Image captionVajiralongkorn ana mtoto mmoja wa kiume aliyempata na mke wake wa zamani Srirasmi
Mpaka sasa haijafahamika wazi, ni uhusiano wa namna gani mfalme huyo mtarajiwa atakuwa nao baina yake na vikosi vya jeshi la serikali ambavyo hivi karibuni vilikuwa vinaiongoza Thailand, ama ni namna gani atapokelewa na raia wake.
Vajiralongkorn katika mbio za baiskeli mwaka 2015
Image captionVajiralongkorn katika mbio za baiskeli mwaka 2015
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment