Breaking News......PIGO JINGINE KWA VIONGOZI WA KITAIFA.....Mbunge wa Dimani CCM. Hafidh Ali Tahir amefariki dunia katika Hospitali ya General huko Dodoma kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na ofisi ya Bunge zinasema alifariki saa tisa usiku wa kuamka leo


Image result for Hafidh Ali Tahir
Mbunge wa Dimani CCM. Hafidh Ali Tahir amefariki dunia katika Hospitali ya General huko Dodoma kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na ofisi ya Bunge zinasema alifariki saa tisa usiku wa kuamka leo. Taarifa za maziko yake zitaelezwa baadae. Mwenyeenzi Mungu amsamehe madhali yake na ampe kauli thabit. Ameen.

Pia Mh. Hafidh Tahir Ally alikuwa mwamuzi wa FIFA na mwana-Yanga ya Kimataifa kindakindaki na ni jana tu amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Tawi la wabunge wanaYanga Dodoma chini ya Uenyekiti wa Venance Mwamoto

Innalilah Waina ilain Rajiun
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment