Afrika yamuomboleza Fidel Castro


Fidel CastroImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionKuhusika kwa Fidel Castro(kushoto) ndani ya masuala ya Afrika kulithihirika
AFRIKA YAMULILIA COMRADE FIDEL CASTRO WASEMA ALIKUWA RAFIKI WA KWELI WANAAFRIKA NA MWANA MAPINDUZI 
Habari za kifo cha Fidel Castro zimeibua hisia za majonzi na huzuni katika maeneo mengi Afrika, hasa kutokana na alivyolifaa bara hili.
Alikuwa mtu aliyekuwa mfano wa kuigwa katika harakati za baada ya uhuru kote barani kwamba wakati mmoja alijielezea kama "sababu nzuri zaidi ya kuwepo kwa binadamu".
Uhusiano wake wa karibu hususan na taifa la Afrika kusini - na vita dhidi ya ubaguzi wa rangi - umekuwa ukiheshimiwa kwa kiasi kikubwa.
Wanajeshi wengi wa Cuba walipoteza maisha yao mbali na nchi yao katika nchi kama vile Angola, wakipigana vita vya ukombozi wa Afrika.
Alisaidia pia wapiganiaji uhuru Msumbiji, kando na kufadhili ujenzi wa miradi mingi ya kuwafaa wananchi mataifa mbalimbali barani Afrika.
Baadhi wanaamini kwamba wakati watu muhimu wa karne ya 20 wanapokumbukwa, ni mmoja wa wanaofaa kukumbukwa.
Wakati wa kutolewa kwa usaidizi wa kimataifa katika kukabiliana na mlipuko wa Ebola katika mataifa ya magharibi mwa Afrika, Fidel Castro, aliwatuma takriban madaktari 300 wa ziada na wauguzi katika mataifa yaliyoathiriwa.
Leonardo FernandezImage copyrightREUTERS
Image captionLeonardo Fernandez alikuwa mmoja wa madaktari wa Cuba waliojitolea kwenda Afrika magharibi
Pia alisema kuwa Cuba iko tayari kusaidiana na Marekani katika masuala ya maslahi ya amani ya dunia.
Tangazo hilo lilitolewa baada ya rais Obama kuwataka Wamarekani kuepuka kupotosha ukweli juu ya Ebola
Katika kipindi cha miongo kadhaa, Castro alituma madaktari wa Cuba katika nchi za kigeni kuwatibu maskini wakiwemo wakazi wa bara la Afrika.
Mbali na Matibabu mapenzi ya Castro kwa Afrika yalidhihirika kusini mwa Afrika pale ilipoingilia katika katika vita vya Angola suala lililobadili sababu ya historia.
Binafsi Castro aliongoza harakati za kivita katika Cuito Cuanavale manamo mwaka 1988 ambapo majeshi ya Cuba yalishinda jeshi la Afrika Kusini na matokeo yake majeshi ya Afrika Kusini hayakuondoka Angola pekee bali Namibia pia ilifanikiwa kupata uhuru wake.
Nelson Mandela binafsi alisema kuachiliwa kwake kutoka gerezani na kushindwa kwa ubaguzi wa rangi kulitokana na matukio ya Cuito Cuanavale.
Mwanajeshi wa Cuba na mwenzake wakivuta sigara nchini AngolaImage copyrightAFP
Image captionMwanajeshi wa Cuba (kushoto) na akivuta sigara nchini Angola
Fidel Castro na Nelson MandelaImage copyrightREUTERS
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ni miongoni mwa viongozi wa kwanza wa nchi mbalimbali duniani waliotuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Fidel Castro.
"Rais Castro alijihusisha na vita vyetu dhidi ya utawala wa ubaguziw a rangi. Aliwahimiza raia wa Cuba kuungana nasi katika vita vyetu dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi," amesema.
Afrika Kusini ilipojipatia uhuru 1994, Cuba na Afrika Kusini chini ya Rais Castro na Rais Mandela zilikuwa na urafiki wa karibu na wa dhati.
Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) Dlamini Zuma pia ametuma rambirambi, kupitia Twitter ambapo amesema Umoja wa Afrika "unasimama kwa pamoja, kama ilivyo kawaida, na watu wa Cuba wanapoomboleza kufuatia kifo cha kiongozi wao Fidel Castro".
BBC
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment