Waziri Nnauye azindua Wiki ya Maonyesho ya Utamaduni wa China Jijini Dar es Salaam

Waziri Nnauye azindua Wiki ya Maonyesho ya Utamaduni wa China Jijini Dar es Salaam

Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Ushirikiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na China katika nyanja mbalimbali zikiwemo za Sanaa na Utamaduni umekuwa chachu kubwa katika kuwajengea uwezo wasanii wetu na kutekeleza shughuli za kimaendeleo zinazofanywa na wataalamu kutoka pande hizi mbili.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokua akizindua wiki ya Maonyesho ya Utamaduni wa China katika Ukumbi wa Utamaduni wa watu wa China leo jijini Dar es Salaam.

 “Kwa miaka mingi Tanzania na China zimekuwa na ushirikiano uliotoa fursa kwa watu wake kujifunza shughuli za sanaa na kiutamaduni zilizoko katika kila nchi hivyo kuendeleza na kuuenzi ushirikiano uliopo katika sekta za Sanaa na Stamaduni” amesema Mhe. Nnauye

Mhe. Nnauye amesema kuwa ushirikiano wa nchi hizi mbili umeweza kukua, kuboresha na kuendeleza wasanii wetu hasa katika kipindi hiki cha maonyesho ambapo hutoa nafasi kwa wasanii wa Tanzania kujifunza mambo mbalimbali ya kiutamaduni na kuwapa wasanii wa hapa nchini fursa ya kufanya maonyesho kama haya nchini China.

Kwa upande wake Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong amesema kuwa Maonyesho ya Utamaduni wa China hapa nchini yanatoa fursa nzuri kwa wananchi wa Tanzania kuelewa na kujifunza utamaduni na sanaa ya China, kuimarisha ushirikiano wa utamaduni wa China na Tanzania pamoja na kukuza urafiki wan chi hizi mbili.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni kutoka Jiangxi China Bw. Chen Hongmin amesema kuwa China itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kubadilishana uzoefu kwa sekta ya Sanaa na Utamaduni na kujifunza mambo mapya ili kuendeleza Utamaduni, ushirikiano na uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili.

Wiki ya Maonyesho ya Utamaduni wa China itakuwa na maonyesho mbalimbali kama vile maonyesho ya sarakasi ya Kichina, maonyesho ya picha, hadhara za opera za China, Udaktari wa kijadi wa China na Utamaduni wa mazoezi maalumu yanayojenga afya yaitwayo Qigong.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akikagua picha mbalimbali za kiutamaduni wa China wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. (katikati mbele) ni Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong.
 Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokua akikagua picha mbalimbali za kiutamaduni wa China wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Wei.
 Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokua akikagua picha mbalimbali za kiutamaduni wa China wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Wei.
 Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Wei akizungumza na washiriki wa maonyesho (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong akizungumza na washiriki wa maonyesho (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na washiriki wa maonyesho (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya washiriki wa Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni wa China wakifuatilia kwa makini matukio mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto waliokaa ni Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong
 Kikundi cha Utamaduni na Sanaa cha Jiangxi kikionyesha sarakasi wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam.
 Msanii kutoka China akionyesha mchezo wa utamaduni wa mazoezi maalumu yanayojenga afya yaitwayo Qigong wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong (wapili kulia) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Wei na wapili kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni kutoka Jiangxi China Bw. Chen Hongmin
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong (wapili kulia) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Wei na wapili kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni kutoka Jiangxi China Bw. Chen Hongmin
Washiriki wa Maonyesho ya wiki ya Utamaduni wa China kutoka Chama cha Mchezo wa WUSHU Tanzania katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM

 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) akimsikiliza Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong (kulia) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni kutoka Jiangxi China Bw. Chen Hongmin.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment