Wananchi Colombia wapinga makubaliano ya amani


Raia wa Colombia wakishangazwa na matokeo ya kura ya maoni
Image captionRaia wa Colombia wakishangazwa na matokeo ya kura ya maoni
Wapiga kura nchini Colombia wamepinga katika kura ya maoni makubaliano ya kihistoria yaliyofikiwa baina ya serikali ya nchi hiyo na kundi la waasi la FARC.
Zaidi ya watu milioni kumi na tatu wamepiga kura, lakini wanaopinga makubaliano hayo wameshinda kwa kura zisizozidi elfu sitini.
Rais Juan Manuel Santos ambae ametia saini makubaliano hayo wiki iliyopita katika sherehe zilizofana na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo kiongozi wa FARC, amesema hatojiuzulu.
Baadhi ya wananchi wa Colombia wakishangilia matokeo ya kura ya maoni
Image captionBaadhi ya wananchi wa Colombia wakishangilia matokeo ya kura ya maoni
Ameongeza kusema, makubaliano hayo ya amani ambayo yatamaliza mgogoro wa miongo mitano bado yanafanya kazi na kwamba yeye atasimamia amani hadi siku yake ya mwisho ofisini.
Kwa upande wake, kiongozi wa kundi la waasi FARC leader, Timochenko, amesikitishwa na matokeo hayo na kusisitiza kwamba yeye pia anataka amani.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment