Viongozi wa IS waondoka katika mji wa Mosul, Iraq


Kuna vijiji 70 ndani ya mjini wa Masul
Image captionKuna vijiji 70 ndani ya mjini wa Masul
Jeshi la Marekani linasema kuna viashiria vinavyoonesha kuwa viongozi wa kundi la Islamic State wameondoka katika mji wa Mosul wakati vikosi vya jeshi la serikali ya Iraq na washirika wake wakikaribia mji huo.
Mkuu wa hilo jeshi Gray Volesky amesema kikosi chake kimeona ishra kwamba wapiganaji wa IS wameondoka katika mji huo.
Lakini amesema alitarajia kuwakuta baadhi ya wapiganaji wa kigeni wa kundi la IS kwa sababu ingekuwa vigumu kwao kukimbia ukilinganisha na wapiganaji wenyeji wa Iraq.
Ameongeza kuwa kunauwezekano wa kutokea mapigano Mosul lakini vikosi vya ulinzi vya Iraq vimeendelea kusonga mbele.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment