DUNIA NZIMA YAMZIKA SHUJAA WA ISRAEL..Viongozi wamlimbikizia sifa Shimon Peres mazishini Jerusalem


Walinzi wa bunge la IsraelImage copyrightAP
Image captionWalinzi wa bunge la Israel wabeba jeneza lenye maiti ya Bw Peres
Viongozi mashuhuri duniani wamemsifu rais wa zamani wa Israel Shimon Peres, ambaye amezikwa leo siku tatu baada yake kufariki akiwa na umri wa miaka 93.
Waziri Mkuu wa israel Benjamin Netanyahu amemweleza kama "mtu muhimu kwa dunia".
Rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwepo kwa kiongozi wa Wapalestina Mahmoud Abbas katika mazishi hayo ni ukumbusho wa "shughuli ambayo haijakamilishwa ya kutafuta amani".
Bw Abbas amekuwa miongoni mwa wageni mashuhuri kutoka nchi za nje waliohudhuria mazishi hayo Jerusalem.
Usalama uliimarishwa na polisi wanasema watu kadha walikamatwa.
Akihutubu wakati wa mazishi hayo, Bw Netanyahu amesema ingawa Israel na dunia yote kwa jumla watu wanamuomboleza Peres, ameacha matumaini duniani.
"Shimon aliishi maisha yenye lengo," amewaambia waombolezaji katika makaburi ya Mlima Herzl, Jerusalem.
"Alipanda na kufikia makuu. Aligusa wengi kwa maono yake na tumaini. Alikuwa mtu humo kwa Israel. Alikuwa mtu muhimu kwa dunia."
'Mwenye kuota zaidi'
Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, aliyesaidia kufanikisha mikataba ya amani ya Oslo kati ya Israel na Wapalestina mapema miaka ya 1990 jambo lililopelekea Shimon Peres kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel, amesema kiongozi huyo alikuwa Mwisraeli "mwenye kuota zaidi".
"Alifikira sana mambo ambayo wengine wetu tungefanya. Alianza maisha kama mwanafunzi mwerevu zaidi wa Israel, alikuwa baadaye mwalimu wake bora zaidi na baada ya hapo mtu mwenye kuota zaidi."
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuImage copyrightAP
Image captionWaziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Rais Barack Obama amemlinganisha Bw Peres na watu wengine mashuhuri wa karne ya 20 ambao amesema alifanikiwa kukutana nao. Wengine amesema ni Nelson Mandela na Malkia Elizabeth wa Uingereza.
Bw Obama pia amemtaja Bw Abbas ambaye ameonekana kupeana mkono na kuzungumza kwa muda mfupi na Bw Netanyahu. Mara ya mwisho wawili hao kukutana hadharani ilikuwa 2010.
Juhudi za kutafuta amani zilitishwa Aptili 2014.
Bw Abbas alikuwa mmoja wa washiriki wa mazungumzo ya amani upande wa Palestine Liberation Organisation (PLO), mjini Oslo na ndiye aliyetia saini mkataba huo mwaka 1993.
Afisa mmoja mkuu wa Wapalestina ameambia shirika la habari la AP kwamba alitaka kutuma ujumbe mzito kwa Waisraeli kwamba Wapalestina wanataka amani na wanafurahia juhudi za wapenda amani kama vile Shimon Peres.
Shimon Peres (kushoto) Mahmoud Abbas (kati) na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Misri Amr Moussa miezi michache baada ya kutiwa saini kwa mkataba wa OsloImage copyrightAP
Image captionShimon Peres (kushoto) Mahmoud Abbas (kati) na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Misri Amr Moussa miezi michache baada ya kutiwa saini kwa mkataba wa Oslo
Msemaji wa Hamas, kundi la Wapalestina lenye msimamo mkali ambalo hutawala Gaza, alikuwa amemtaka Bw Abbas "kutohudhuria mazishi ya mhalifu Shimon Peres".
Bw Peres hulaumiwa kutokana na urushaji wa mabomu 1996 katika eneo la Qana kusini mwa Lebanon ambao ulisababisha vifo vya watu 100 waliokuwa wametafuta hifadhi kambi ya Umoja wa Mataifa.
Ulinzi mkali umewekwa mjini JerusalemImage copyrightREUTERS
Image captionUlinzi mkali umewekwa mjini Jerusalem
Bw Barack Obama akihudhuria mazishi hayoImage copyrightREUTERS
Image captionBw Barack Obama akihudhuria mazishi hayo
Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton ambaye alisaidia kupatikana kwa Mkataba wa amani wa OsloImage copyrightEPA
Image captionRais wa zamani wa Marekani Bill Clinton ambaye alisaidia kupatikana kwa Mkataba wa amani wa Oslo
Mwanamfalme Charles wa Uingereza na Rais Francois Hollande wa UfaransaImage copyrightREUTERS
Image captionMwanamfalme Charles wa Uingereza na Rais Francois Hollande wa Ufaransa

Wageni mashuhuri waliohudhuria:
 • Barack Obama, Rais, Marekani
 • Bill Clinton, rais wa zamani, Marekani
 • Mwanamfalme Charles, Uingereza
 • Boris Johnson, Waziri wa mambo ya nje, Uingereza
 • Tony Blair, waziri mkuu wa zamani, Uingereza.
 • Malcolm Turnbull, Waziri Mkuu, Australia
 • Justin Trudeau, Waziri Mkuu, Canada
 • Donald Tusk, Rais, Baraza la Umoja wa Ulaya
 • Francois Holland, Rais, Ufaransa
 • Joachim Gauck, Rais, Ujerumani
 • Matteo Renzi, Waziri Mkuu, Italia
 • Jenerali Nakatani, waziri wa zamani wa ulinzi, Japan
 • Jawad Anani, waziri wa ngazi ya juu, Jordan
 • Enrique Pena Nieto, Rais, Mexico
 • Jens Stoltenberg, Katibu Mkuu, Nato
 • Mark Rutte, Waziri Mkuu, Uholanzi
 • Valentina Matviyenko, spika, bunge la juu, Urusi
 • Mfalme Felipe VI, Uhispania
 • Ban Ki-moon, Katibu Mkuu, Umoja wa Mataifa

Shimon Peres alikuwa nani?

 • Alizaliwa 1923 Wisniew, Poland, eneo ambalo sasa hufahamika kama Vishneva, Belarus
 • Alichaguliwa kwenye Knesset (Bunge la Israel) mara ya kwanza mwaka 1959
 • Alihudumu katika serikali 12, mara moja kama rais na mara mbili kama waziri mkuu.
 • Alitazamwa kama mpenda vita miaka yake ya awali - aliongoza mashauriano ya kuitafutia silaha Israel ilipokuwa bado taifa changa
 • Alikuwa kwenye serikali iliyoidhinisha sera ya kujengwa kwa makazi ya Wayahudi katika maeneo ya Wapalestina yaliyotekwa na Israel
 • Hata hivyo, alitekeleza mchango muhimu katika kupatikana kwa Mkataba wa Amani wa Oslo, mkataba wa kwanza kati ya Israel na Wapalestina, uliosema wangefanya juhudi "kuishi kwa amani pamoja"
SHARE

 • Image
 • Image
 • Image
 • Image
 • Image
  Blogger Comment
  Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment