Breaking News.... Watu 12 wauawa shambulio la al-Shabaab Mandera, Kenya


Washambuliaji walirusha vilipuzi kwenye jumba hiloImage copyrightIBRAHIM ADAN ALI / KEY FM
Image captionWashambuliaji walirusha vilipuzi kwenye jumba hilo

Breaking News....

Watu 12 wauawa shambulio la al-Shabaab Mandera, Kenya

Watu 12 wameuawa baada ya watu wenye silaha kushambulia nyumba moja ya malazi mjini Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya.
Msemaji wa serikali ya Kenya Eric Kiraithe amesema watu sita wameokolewa kutoka kwenye hoteli hiyo ya Boshari.
Wanamgambo wanaoaminika kuwa wa kundi la al-Shabaab walishambulia nyumba hiyo mwendo wa saa tisa unusu usiku. Walirusha vilipuzi kwenye nyumba hiyo kabla ya kuingia ndani na kuanza kuwafyatulia risasi waliokuwemo ndani.
"Sehemu ya jumba iliporomoka, na kuua watu 12. Watu sita wametolewa kutoka kwenye vifusi vya jengo hilo wakiwa hai kufikia sasa," ameandika Bw Kiraithe kupitia mtandao wa Twitter.
Wataalamu wa mabomu wanafanya uchunguzi kubaini ni vilipuzi vya aina gani vilitumiwa kutekeleza shambulio hilo.
Mandera
Image captionMji wa Mandera unapatikana katika mpaka wa Kenya, Somalia na Ethiopia
Kundi la al-Shabaab limekiri kutekeleza shambulio hilo.
Mji wa Mandera umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa al-Shabaab, kundi linalopigana dhidi ya serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa katika taifa jirani la Somalia.
Wanamgambo hao wamekuwa wakishambulia watu ambao si wa asili ya Kisomali.
Maafisa wa usalama nje ya hoteli ya BishaaroImage copyrightIBRAHIM ADAN ALI / KEY FM
Image captionMaafisa wa usalama nje ya hoteli ya Bishaaro
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment