Breaking News... Simba Na Yanga marufuku kutumia UWANJA WA TAIFA Pia Simba kutopata Mgao WA mechi ya jana


TAARIFA MUHIMU..!

 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo asubuhi ya leo tar 02/10/2016 ametembelea uwanja wa Taifa na kukagua uharibifu uliofanywa na mashabiki wa Simba katika mechi dhidi ya Yanga hapo jana. Yafuatayo ni maamuzi yaliyochukuliwa na Serikali:

1)Simba na Yanga hazitoruhusiwa kutumia uwanja wa taifa hadi hapo itakapo amuliwa vinginevyo.

2)Simba itatakiwa kulipia hasara iliyotokana na uharibifu huu.

3)Simba haitopata mgao wake wa mechi ya jana.

4)Kamera za CCTV zitafungwa uwanja mzima kufuatia mienendo ya mashabiki wanapokuwa uwanjani ili kuweza kuwatambua watu wote watakao jihusisha na vitendo vya fujo.

SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment