WALIOSOMA KILAKALA SEKONDARI WACHANGISHANA FEDHA , WAKARABATI JENGO LA ZAHANATI , WANUNUA SHUKA NA MAGODORO , MADAFTARI

WAHITIMU waliosoma Shule ya Sekondari Kilakala , iliyopo mkoani Morogoro wameombwa kujitokeza kuunga mkono mpango wa Serikali wa uimalishaji wa miundombinu ya elimu itakayoweka mazingira mazuri yatakayowavutia wanafunzi kusoma. 
Rai hiyo imetolewa na wahitimu wa mwaka wa masomo  1986 hadi 1995 ambao wameanzisha   umoja wao ukiwa na  lengo la  kusidia utatuzi wa changamoto mbalimbali ikiwemo  uboreshaji  wa huduma za afya kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Muhitimu wa zamani wa  shule hiyo , Wanyenda Kuta , aliyeambatana na wenzake 15  waliosoma kwenye  hiyo ya  wasichana  wenye vipaji maalumu , Augosti 27, mwaka huu alisema,  shule ya Kilakala   imetoa wahitimu wengi wanawake.
Alisema  , asilimia kubwa ya waliohitimu katika shule hiyo ni watumishi katika ngazi mbalimbali za Kiserikali , Viongozi wa kisiasa , Mashirika ya Umma ,  Sekta binafsi  na wajasilimali wakubwa .
Hivyo alisema , wao  walipita katika mikono salama ya shule, walimu ,wazazi  na Serikali na  kwa sasa  wanao wajibu wa kurudisha  kidogo wanachokipata  kwa kusaidiana na Serikali kwenye  mpango  yake ya kuboresha miundombinu ya elimu ikiwemo katika shule hiyo. 

“ Kufika kwetu hapa  kumetokana na wananchi kulipa kodi za Serikali ambayo ilijenga shule hii  ambayo imetuwezesha sisi kupata elimu bora hapa Kilakala” alisema Kuta.
Hivyo alisema , kwa kutambua umuhimu huyo, wahitimu hao waliamua kuchangishana fedha na kupatikana kiasi cha Sh milioni tatu  zilizosaidia kununua shuka, magodoro  na ukarabati wa Zahanati ya Shule ili hiyo.

Pamoja na hayo ,alitumia nafasi hiyo  kuwasihi  wanafunzi wakike wanaosoma katika shule hiyo wajitambue kuwa  wanaowajibu nao  kuja kulisaidia  taifa lao kwa vile  Serikali inatumia kodi za wananchi katika kuboresha mazingira ya elimu nchini.
“ Kilakala Sekondari imetoa na itaendelea kutoa  wataalamu  wa fani mbalimbali nchini , na  wale ambao ni matunda ya shule hii tuangalie tulikotoka  “ alisema Kuta na kuongeza kuwa.

“ Jambo ambalo tunaweza kulifanya ni kuchangia kuboresha shule yetu ikiwezekana kuanzisha siku maalumu kwa wote waliosoma hapa ili michango yetu isaidia kuboresha shule hii , tunao  baadhi ya  viongozi wa ngazi za juu serikalini wakiwemo mawaziri ” alisema Kuta.

Kwa upande wake Kiranja mkuu wa shule hiyo, Gema Kataraiya, pamoja na Kiranja wa Afya kwa nyakati tofauti waliwapongeza wahitimu hao kwa kutoa mashuka na kukarabati jengo la Zahanati ya shule hiyo'

Pamoja na ukarabati wa Zahanati hiyo, wanafunzi hao walisema bado kuna upungufu mkbwa wa vifaa vya kutolea huduma vikiwemo vipimo vya malaria na mazingira yasiyo rafiki ya  vyoo.
 Awali,  Makamu Mkuu wa Shule hiyo upande wa Taaluma, Mussa Katunzi, alisema kuwa mchango uliotolewa na wahitimu hao ni moja ya chachu ya kuwavuta wengine aliosoma shule hiyo kuona nao wanaowajibu wa kuchangia maendeleo ya elimu .

Baadhi ya wahitimu wa mwaka 1986 hadi 1995 wa  shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kilakala , inayomilikiwa na Serikali ambao wameunda  umoja wao  wakiimba wimbo wa shule ikiwa ni ishara ya kukumbuka walipokuwa wanafunzi shuleni hapo  baada ya kufika shuleni hapo  Augosti 27, mwaka huu kukabidhi msaada shuka na madogoro kwa ajili ya Zahanati ya shule ambayo  pia ilikarabatiwa na  michango yao.
...............................
 Baadhi ya wahitimu wa mwaka 1986 hadi 1995 wa  shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kilakala , inayomilikiwa na Serikali ambao wameunda  umoja wao  wakiekelea jengo la  Ofisi ya Mkuu wa shule kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni.
 Mhitimu wa shule  ya Sekondari Kilakala , Claudia Iringo akimkaabidhi mwanafunzi wa shule hiyo madafyari  kwa ajili ya  wenzao wenye mahitaji maalumu , wahitimu hao wa zamani wapatao 15  waliosoma kuanzia 1988 hadi 1995  waliitembele shule yao Augosti 27, mwaka huu .
 Baadhi ya wahitimu wa mwaka 1986 hadi 1995 wa  shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kilakala , inayomilikiwa na Serikali ambao wameunda  umoja wao  wakiwa katika Ofisi ya Mkuu wa shule kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni  wa shule baada ya kufika shuleni hapo  Augosti 27, mwaka huu kukabidhi msaada shuka na madogoro kwa ajili ya  Zahanati ya shule ambayo  pia ilikarabatiwa na  michango yao.

 Wanafunzi wa   shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kilakala,inayomilikiwa na Serikali wakifurahia kuona  wahitimu  wa zamani katika shule hiyo wamewakumbuka  kwa kutoa  kmsaada shuka na madogoro kwa ajili ya  Zahanati ya shule  na kulikarabati   jengo hilo.
 Picha ya pamojana mwalimu na viongozi wa wanagfunzi
 Wahitimu wakiangalia shughuli za shule yao
 Baadhi ya wahitimu wa mwaka 1986 hadi 1995 wa  shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kilakala , inayomilikiwa na Serikali ambao wameunda  umoja wao  wakiimb na kicheza kukumbusha enzi zao katika  shule hiyo.
Baadhi ya wahitimu wa mwaka 1986 hadi 1995 wa  shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kilakala , inayomilikiwa na Serikali ambao wameunda  umoja wao  pamoja na baadhi ya viongozi wa wanafunzi wa shule hiyo, walimu na bodi ya shule wakiwa ndani ya  jengo la zahanati ya  shule  baada ya kukabidhi shuka, magodoro pamoja na madatfari kwa wanafunzi.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment