VIJANA WA 'BUKOBA MPYA' WAMPONGEZA MAMA ANNA TIBAIJUKA KWA KUSHINDA TUZOVijana wa Bukoba Mpya wampongeza Profesa  Anna Tibaijuka kwa ushindi wa Tuzo ya 'HRH Prince Khalifa Bin Salman Al Khalifa Award for Suitanable Development' Sherehe za utoaji wa tuzo hizo umefanyika juzi katika viwanja vya makao makuu ya umoja wa mataifa  jijini New York, Marekani, na kuudhuriwa na viongozi mbalimbali duniani wakiwemo mabalozi, mawaziri  na viongozi waandamizi wa Umoja wa Mataifa.
Bi Happiness Essau,Katibu, Vijana wa Bukoba Mpya akimpongeza Mama Anna Tibaijukakatika kongamano la Bumudeco lililofanyika  mjini Bukoba Desemba  27, 2015 


Salaam za pongezi kwa 
Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka

Tumepokea kwa furaha isiyo kifani taarifa ya ushindi wako wa Tuzo ya 'His Royal Highness Prince Khalifa bin Salman Al Khalifa Award for Sustainable Development'. Ushindi huu ni uthibitisho mwingine juu ya kutambulika kwa juhudi na kuthaminiwa kwa jitihada zako katika kuendeleza makazi.
Tunaona fahari kwa kazi kubwa uliyoifanya kuubadilisha Mtaa wa Kibera nchini Kenya na kwa hakika, halitafutika jina la Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka kwenye miradi mikubwa ya makazi na mazingira inayoendelea kutekelezwa katika nchi za maziwa makuu (Nile Basin Initiatives, Land Reform and Urban Planning, Lake Victoria Environmental Management Programme, n.k).
Toka uhuru, ukiachilia mradi wa SADELIN, Kagera haina kumbukumbu ya kuletewa mradi mkubwa kwa nguvu na jitihada za Serikali. Lakini upo ushahidi usiofutika juu ya jinsi ushawishi wako kwenye ashirika ya kimataifa kama Benki ya Dunia na UNDP ulivyoisaidia Kagera kufikiriwa pamoja na mikoa mingine na hatimaye kupata miradi ya maendeleo.
Nahau za mfumo‐dume husema ‘Omwatani Takweeta Mushaija’ na iko hivyo pia katika maandishi ya Vitabu vitakatifu kwamba ‘Nabii Hakubaliki Nyumbani Kwake na Kwa Watu Wake’ Tunasikitika kwamba haya yote yamekuwa kweli hata kwako pia. Kama tulivyoeleza katika kitubio chetu kwenye mkutano wa BUMUDECO, vijana wa Bukoba Mpya tunajutia zaidi kwamba nasi tulishiriki kukusurubisha pasipo kutafuta kuujua ukweli. Tulipelekwa na upepo wa matukio na tukajinyima nafasi ya kutathmini malengo ya matukio. Tunazidi kukuomba msamaha na kuwaombea wengine wote ambao ukweli haujafunuliwa kwao ikiwemo watakaotusi pongezi hizi. Tunakuahidi kuwa watakao baki katika fikra za zamani ni wale wasiokuwa wetu lakini sisi vijana wa Bukoba Mpya tutasimama daima na watu wetu ikiwemo wewe.
Pamoja na pongezi hizi za jumla, tunaomba mara urejeapo nchini na upatapo muda, ujumuike na uwakilishi wa Bukoba Mpya‐Tawi la Dar es Salaam kwa hafla fupi ya kukupongeza.

Imetolewa na
Happiness Essau
Katibu, Vijana wa Bukoba Mpya
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment