TUMEPATA TAARIFA KUTOKA KWA KATIBU WA MAKAMU WA RAIS (Rajab Waziri) KUWA WANAENDELEA VIZURI MPAKA SASA.

Breaking Newss....Msafara wa makamo wa Rais wapata ajali mda huu majeruhi wakimbizwa Hospitalin....

TUMEPATA TAARIFA KUTOKA KWA KATIBU WA MAKAMU WA RAIS (Rajab Waziri) KUWA WANAENDELEA VIZURI MPAKA SASA. 
Baada ya taarifa ya Ajali  iliyotokea Muda huu.
Msafara wa makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzani Samia suluhu hassani ambao ulikuwa unaelekea wilayani tandahimba ukitokea ikulu ndogo ya rais mtwara umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa ligula.

Ajali imetokea mbele kidogo ya kijiji cha nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya mtwara

Majeruhi walioumia ni dereva  pamoja na wasaidizi wanne wa makamu rais.

Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi wa habari wa channel ten, startv na clouds tv liliacha njia na nusura kupinduka.

Barabara ya kutoka mtwara kuelekea tandahimba si ya kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment