Mpiganaji wa Kiislamu kutoka Mali Al Mahdi afungwa jela ICC.. Ni yule aliyeongoza kuvunjwa kwa mji wa kihistoria wa Timbuktu

 

Ahmad Al Faqi Al MahdiImage copyrightAFP
Image captionAhmad Al Faqi Al Mahdi alikiri mashtaka
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) imemhukumu mwanamgambo wa Kiislamu raia wa Mali Ahmad Al Faqi Al Mahdi kifungo cha miaka tisa jela.
Al-Mahdi alikuwa ameshtakiwa makosa ya uhalifu wa kivita kuhusiana na kuharibiwa kwa makaburi tisa na msikiti mashuhuri katika mji wa kale wa Timbuktu, 2012.
Wakati wa kusikizwa kwa kesi yake, Al Faqi Al Mahdi alikiri mashtaka.
Kesi dhidi yake ilisikizwa siku chache tu kwa sababu yake kukiri mashtaka.
Mshtakiwa ni mwalimu wa kidini na anadaiwa kuamrisha wapiganaji wa kundi la Kiislamu la
Ansar Dine waharibu turathi na maeneo ya kidini Timbuktu kati ya 2012 na 2013.
Al Mahdi kuhukumiwa mahakama ya ICC
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment