Mourinho: Man City watakuwa hatari bila Sergio Aguero


Sergio AgueroImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionAguero anatumikia marufuku kwa kumchezea visivyo Winston Reid wa West Ham

Mourinho: Man City watakuwa hatari bila Sergio Aguero

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema itakuwa vigumu kucheza dhidi ya Manchester City wakiwa bila Sergio Aguero Jumamosi.
Mshambuliaji huyo wa Argentina, 28, amepigwa marufuku kucheza mechi tatu baada ya kumgonga mchezaji wa West Ham kwa kiwiko cha mkono mechi ambayo City walishinda 3-1.
Aguero amefunga mabao matatu katika mechi tatu alizocheza Ligi ya Premia msimu huu lakini Mourinho anasema kutokuwepo kwake kuna maana kwamba City, chini ya Pep Guardiola hawataweza kutabirika.
"Akiwa hachezi, basi wana wachezaji wengine wengi wanaweza kutumia," amesema Mourinho.
"Inakuwa vigumu zaidi. Sergio Aguero akiwepo basi unajua atacheza, na unajua watajipanga vipi."
Mourinho amesema mmoja kati ya Kelechi Iheanacho, Raheem Sterling na David Silva anaweza kuchezeshwa kama 'nambari tisa bandia' kwenye debi hiyo Old Trafford.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment